Friday, December 26, 2014

Unamfahamu mchezaji anayeichukia Krismasi?

ronnie tweet
Wachezaji wengi wa soka barani ulaya wamekuwa mstari wa mbele kuwatakia mashabiki wao heri ya sikukuu ya krismasi katika kipindi hiki ambacho kila mmoja amekuwa katika mzuka wa sikukuu hii .
Wayne Rooney hakubaki nyuma kwa kutumia mtandao wa twitter kuwatakia mashabiki wake heri ya sikukuu .
Wayne Rooney hakubaki nyuma kwa kutumia mtandao wa twitter kuwatakia mashabiki wake heri ya sikukuu .
Wachezaji hawa kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kama Facebook , Twitter na Instagram wamekuwa wakionyesha ubinadamu wao kwa kutuma ujumbe wa aina mbalimbali wa kuwataka mashabiki wao kuwa na furaha katika kipindi hiki .
Wachezaji wa Juventus ya Italia wakiwatakia mashabiki wao heri ya Christmas.
Wachezaji wa Juventus ya Italia wakiwatakia mashabiki wao heri ya Christmas.
Kwa beki raia wa Ujerumani anayecheza kwenye klabu ya Stoke City Robert Huth hali imekuwa tofauti baada ya mchezaji huyo kuonyesha hisia za kinyume kabisa na wachezaji wengine .
Mchezaji huyu aliustaajabisha ulimwengu kwa kitendo chake cha ku-tweet hisia zake kuhusiana na sikukuu hii ambayo inadhimishwa ulimwenguni kote.
Tweet inayoonyesha hisia za beki Robert Huth kwa sikukuu ya Christmas.
Tweet inayoonyesha hisia za beki Robert Huth kwa sikukuu ya Christmas.
Robert Huth kwa kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter aliandika kuwa anaichukia krismasi na hakutoa sababui za msingi za chuki aliyo nayo kwa sikukuu hii .
Hakuna aliyeweza kufahamu chanzo hasa cha utofauti huu toka kwa beki huyu Mjerumani ambaye amejijengea sifa kama beki mgumu asiyetetereshwa na washambuliaji awapo uwanjani .

Umeisikia hii ya waliotaka kuiba sanamu la Bikira Maria kanisani?

MarVijana watatu Songea wametakiwa kwenda na wazazi wao kutubu dhambi za kutaka kuiba sanamu la Bikira Maria katika Kanisa Katoliki la Kigango cha Samora.
Katekista wa Kigango hicho Keneth Mhagama walisema vijana hao walifanya jaribio hilo usiku wa manane baada ya ibada ya mkesha ambapo walinzi walifanikiwa kuwadhibiti kabla hawajafanikiwa na wakawekwa mbaroni.
Vijana hao ni Ahmed, Mohammed na Leonard ambapo Padri wa Kanisa hilo Cristom Kapinga amesema vijana hao wanatakiwa kutubu la sivyo watawaacha kwenye mikono ya sheria washughulikiwe.
Chanzo cha Habari: Gazeti Mtanzania, December 26.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Simba bado kiza kinene.

MASHABIKISIMBA
Ligi kuu ya soka ya Tanzania bara imerejea hii leo baada ya mapumziko ya mwezi mmoja na nusu wakati ligi hiyo iliposimama .
Katika mchezo uliopigwa hii leo , wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club walianza vibaya nusu ya pili ya mzunguko wa kwanza baada ya kukubali kipigo cha bao moja bila .
Bao hilo pekee lilifungwa kwenye dakika ya 21 na  mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Coastal Union Atupele Green ambaye alifanyia kazi makosa ya kipa wa Simba Ivo Mapunda na beki Mohamed Hussein .
Kwa matokeo haya Kagera Sugar wamefikisha pointi kumi na tatu baada ya michezo nane na wanapanda mpaka kwenye nafasi ya nne .
Ligi hiyo itaendelea hapo kesho kwa michezo miwili ambapo Jkt Ruvu na Ruvu Shooting watacheza huko Azam Complex Chamazi , na Tanzania Prison watacheza na Coastal Union huko Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.

 0


MWAKA 2014 unakatika, matukio ya kukumbukwa ni pamoja na wasanii Bongo kupoteza maisha katika mazingira yasiyotarajiwa, Ijumaa linakupa hatua kwa hatua.Kumbukumbu za haraka zinabainisha kuwa, tangu mwaka 2011 mpaka 2014, wasanii  wenye majina makubwa na madogo wasiopungua 32 wamefariki dunia kwa sababu mbalimbali.
Inauma sana! Katika kipindi cha miaka mitatu kuwapoteza wasanii kwa kiasi hicho ni pigo kubwa kwa tasnia, hasa filamu na muziki, ukiwemo wa muziki wa Injili.
Leo katika toleo hili maalum, Ijumaa linawakumbusha wasanii hao walioaga dunia na namna vifo vyao vilivyotokea.
ALBERT MANGWEHA ‘NGEA’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza  ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6, 2013.
LANGA KILEO ‘RAIS WA GHETO’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Alifariki dunia Juni 13, 2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar akiwa na miaka 28. Kifo chake kilithibitishwa kuwa, kilitokana na kuzidiwa na Ugonjwa wa Malaria. Alizikwa  Juni 17, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
MUHIDIN GURUMO ‘MAALIM’
Alikuwa mkongwe wa muziki wa dansi Bongo. Mpaka kifo chake kilichotokea Aprili 13, mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na miaka 74, alikuwa mwanamuziki wa Msondo Music Band. Kifo chake kilisababishwa na kusumbuliwa na matatizo ya moyo. Alizikwa Aprili 15 kwenye Makaburi ya Kijiji cha Masaki, Kisarawe, Pwani.
FATUMA BINTI BARAKA ‘BI KIDUDE’
Alikuwa mwanamuziki wa taarab. Alifariki dunia Aprili 17 2013 Bububu mjini Zanzibar akiwa na miaka inayodaiwa haipungui mia moja. Alizikwa siku iliyofuata, kwenye Makaburi ya Bububu, Zanzibar.
SHEM IBRAHIM KALENGA
Alikuwa mwanamuziki wa dansi. Alifariki dunia Desemba 15, mwaka huu kwenye Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam akiwa na miaka 64. Haijathibitishwa ugonjwa uliomuua. Alizikwa Desemba 16 kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.
MWANAISHA MOHAMED MBEGU ‘AISHA MADINDA’
Alitikisa kwenye eneo la unenguaji kwenye bendi ya muziki wa dansi. Alifariki dunia Desemba 17, mwaka huu Mwananyamala, Dar es Salaam akidaiwa kuchomwa sindano yenye madawa ya kulevya kiasi cha kuwa sumu kali mwilini. Alizikwa Desemba 19 kwenye Makaburi ya Kigamboni jijini Dar. Mpaka kifo chake alikuwa na miaka 35.
SUDI MOHAMED ‘MCD’
Alikuwa mpiga tumba kwenye Bendi ya The Afrcan Stars ‘Twanga Pepeta’. Alifariki dunia Januari 27, mwaka huu mjini Moshi akisumbuliwa na matatizo ya kifua. Alizikwa Januari 28, mwaka huu kwenye Makaburi ya Njoro, Mjini Moshi.
HAMIS KAYUMBU ‘AMIGOLAS’
Alikuwa mwimbaji wa zamani wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’. Alifariki dunia Novemba 9, 2014 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku kadhaa akisumbuliwa na matatizo ya moyo. Alizikwa Novemba 10, kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar.
STEVEN KANUMBA
Alikuwa msanii nyota wa filamu za Bongo. Alifariki dunia Aprili 7, 2012, Sinza jijini Dar baada ya kuangukia sehemu ya nyuma ya kisogo. Mpaka anaaga dunia, Kanumba alikuwa na miaka 28. Alizikwa Aprili 10, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar akiwa na miaka 28.
MARIAM KHAMIS ‘PAKA MAPEPE’
Alikuwa mwanamuziki wa taarab wa Bendi ya Tanzania One Theatre ‘TOT’. Alifariki dunia Novemba 13, 2012 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar kwa matatizo ya uzazi wakati akijifungua. Alizikwa Novemba 14 kwenye makaburi ya Magomeni, Dar.
GEORGE OTIENO ‘TYSON’
Alikuwa msanii na mwongozaji wa filamu za Bongo. Alifariki dunia Mei 31, mwaka huu kwa ajali ya gari mkoani Morogoro akiwa na miaka 31. Alizikwa Juni 14, Kijiji cha Siaya, Kenya.
AMINA NGALUMA ‘JAPANESE’
Anaitwa Amina Ngaluma. Alikuwa mwimbaji wa bendi mbalimbali nchini ikiwamo Double M Sound na African Revolution. Alifariki dunia Mei 15, mwaka huu nchini Thailand baada ya kupatwa na uvimbe kichwani. Alizikwa jijini Dar, Mei 24, 2014 kwenye Makaburi ya Tabata, Dar.
ADAM KUAMBIANA
Alikuwa msanii wa sinema za Bongo. Alifariki dunia Mei 17, mwaka huu, Sinza jijini Dar baada ya kuugua ghafla. Alizikwa Mei 20, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar akiwa na miaka 38.
RECHO HAULE
Alikuwa msanii wa filamu Bongo. Alifariki dunia Mei 27, mwaka huu kwenye Hospitali ya Lugalo jijini Dar kwa matatizo ya uzazi wakati wa kujifungua akiwa na miaka 26. Alizikwa Mei 30 kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.
ZUHURA MAFTAH ‘MELISA’
Zuhura Maftah ‘Melisa’ (39) alikuwa chipukizi wa Bongo Muvi. Alifariki dunia Septemba 8, 2013 katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani. Alizikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
MZEE MANENTO
Mzee Manento (73) alikuwa msanii wa Bongo Movies. Alifariki dunia Oktoba 29, 2014 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni, Dar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu. Alizikwa kijijini kwake, Mamba-Miamba wilayani Same, Kilimanjaro.
JUMA KILOWOKO ‘SAJUKI’
Sajuki (26) alikuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Januari 1, 2013 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya uvimbe na kansa ya ini. Alizikwa kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.
SAID NGAMBA ‘MZEE SMALL’
Mzee Small (59) alikuwa mkongwe wa vichekesho Bongo. Alifariki dunia Juni 8, 2014 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kusumbuliwa na kiharusi kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye makaburi ya Tabata-Segerea, Dar.
YESAYA AMBIKILE ‘YP’
YP (26) alikuwa msanii wa Bongo Fleva kutoka Kundi la TMK Wanaume Family. Alifariki dunia Oktoba 20, 2014 kwenye Hospitali ya Temeke, Dar baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kifua kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye makaburi ya Chang’ombe, Dar.
AHMED ALLY UPETE ‘GEEZE MABOVU’
Geeze Mabovu alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Alifariki dunia Novemba 12, 2014 baada ya kuumwa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Alizikwa huko Iringa katika makaburi ya Makanyagio.
JOHN STEFANO MAGANGA
Alikuwa mwigizaji wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Novemba 24, 2012 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar baada ya kuugua ghafla. Alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.
JAJI KHAMIS ‘KASHI’
Mwigizaji Kashi alifariki dunia Juni 10, 2013 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar alikokimbizwa baada ya kuzidiwa ghafla. Alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.
RAMADHAN MKIETY ‘SHARO MILIONEA’
Sharo alikuwa ni staa wa vichekesho na Bongo Fleva. Alifariki dunia Novemba 26, 2012 baada ya kupata ajali mbaya huko Muheza, Tanga. Alizikwa kijijini kwao, Lusanga, Muheza mkoani Tanga.
SHERRY MAGALI
Sherry alikuwa mchekeshaji na mwigizaji wa sinema za Kibongo. Alifariki dunia Oktoba 21, 2014 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kuugua kifua kwa muda mrefu. Alizikwa kwenye Makaburi ya Mji Mpya, Morogoro.
Wakati huohuo, taarifa zilizotufikia zinasema kuwa, yule mchungaji aliyewahi kutabiri vifo vya wasanii wawili wa filamu na Bongo Fleva ameibuka tena na kutabiri kuwa, jinamizi la vifo vya wasanii bado lipo ambapo amesema:
“Natabiri tena vifo vya wasanii nchini. Kwamba, hadi kufikia Februari mwakani (2015), wasanii wawili watapoteza maisha.
“Lakini ili kukwepa mauti wasimame katika roho wakimwomba sana Mungu na kutoa sadaka bila kusahau kuwasaidia yatima na wazee.”
Naye mtabiri maafuru nchini, Maalim Hassan Hussein Yahya amesema roho ya mauti kwa wasanii ipo inazunguka, itafanya kazi hiyo kufikia Aprili mwakani.
Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti Pendwa ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi, Amani, Risasi Mchanganyiko na Risasi Jumamosi tunasema; R.I.P wasanii wetu!  

Wednesday, December 24, 2014

Kati ya Picha Hizi Nne za Mzee Majuto Ipi ni Kali Zaidi?

Kati ya Picha Hizi Nne za Mzee Majuto Ipi ni Kali Zaidi?
    PICHA ni kumbukumbu muhimu katika maisha, hufurahisha na kuburudisha na wakati mwingine uhudhunisha pia ilimradi tu maisha yanasonga mbele. Leo kutoka kwenye maktaba yetu ya picha, tumekutana hizi picha nne za mwigizaji nguli wa filamu za vichekesho hapa nchini, Amri Athuman'King Majuto' ukipenda muite Mzee Majuto alizopiga na waigizaji hawa wakike, Wema Sepetu, Riyama Ally,Kajala Masanja na Jackline Masawe “Wolper”.

    Hii ni Good news kutoka kwa Damian Soul na Joh Makini Mwaka 2015

    .
    Pichani kushoto (Mtayarishaji wa muziki Pancho Latino kutoka B hitz akiwa na Joh Makini & Damian Soul.
    Baada ya hit song Ni Penzi kufanya vizuri kwenye spika za radio yako sasa good news ninayotaka kukupatia ni kwamba usiku wa Dec 23 Mkali wa mtindo wa Soul,Damian Soul  na Mwamba wa Kaskazini Joh Makini wamemaliza maandalizi ya single yao mpya iliyotayarishwa katika studio za B hits chini ya mtayarishaji Pancho Latino ambayo inatarajiwa kutoka rasmi tarehe 1 Jan 2015.
    Damian amehabarisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa twitter na kuandika #Kaa tayari kwa mkao wa kula…1/1/2o15.. @damian_soul2gether with.. blood again @joh_makini #Blessings@pancholatino @hermyb #Hatareeeeeee_kubwa


    Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

    Mabibi na Mabwana Tunda man anakualika kuitazama hii video yake mpya

    .
    .
    Msanii wa  kund la Tip Top Connection Tunda Man baada ya kufanya vizuri kwenye video ya hit song Msambinugwa aliyomshirikisha Ali Kiba time hii anakualika kuitazama hii video yake mpya iitwayo Mapenzi yale yale
    Ukishamaliza kuitazama hapa mtu wangu usisahau kuniandikia ya moyoni ili Tunda Man akipita hapa asome kutoka kwa watu wake wa nguvu..

    Thursday, December 11, 2014

    Chidi Benz ameyaandika haya kuhusu ishu ya Diamond na Davido, Zitto na MwanaFA ni miongoni mwa waliolike.

    Diamond DavidoKuna habari nyingi zinaandikwa sasa hivi kuhusu uhusiano wa Diamond na mwimbaji Mnigeria Davido ambae weekend iliyopita wakati mshindi wa BBA 2014 alipotangazwa kuwa ni Mtanzania Idris aliandika tweet iliyoanzisha tatizo.
    Wengi walimuelewa kama kaidiss Tanzania kwa kumaanisha haikustahili kupata ushindi wa Channel O awards tatu alizoshinda Diamond na vilevile labda haikustahili ushindi wa BBA pia.
    Sasa kutokana na kinachoendelea sasa hivi rapper Chiddi Beenz ameamua kuyatoa yake ya moyoni kupitia page yake ya facebook leo kama inavyosomeka hapa chini baada ya Watanzania kuendelea kumtukana Davido kwenye mitandao yake ya kijamii na hata reaction ya Diamond mwenyewe baada ya kushinda tuzo nyingine Nigeria.
    Diamond NIG
    BenzKama unachochote cha kuongezea kwenye hii post ya Chidi Benz usisitie kuniachia comment yako hapa chini mtu wangu.

    Wednesday, December 10, 2014

    WOLPER: Aonyesha Tatoo Yake Mpya

    WOLPER: Aonyesha Tatoo Yake Mpya
    • WOLPER: Aonyesha Tatoo Yake Mpya 1
    • WOLPER: Aonyesha Tatoo Yake Mpya 2
     
    Hatimaye muigizaji wa filamu, Jackline Wolper akiwa ndani ya mavazi ya ki-TOM BOY, leo hii ameonyesha Tatoo yake mpya aliyopo sehemu ya juu ya mkono wake wa kushoto.
    Hivi majuzi mitandaoni kulikuwa na picha zilizomuonyesha mwanadada huyo akiwa anachorwa tatoo na jamaa wanaofahamika kama MALAIKA TATOO.
    Katika moja ya picha hizo ilimuonyesha Wolper ameketi kwenye kiti cha kibosi ya cha kuchorewa huku amevalia mavazi ya ki-tom boy meusi na bonge la NDULA, huku jamaa mchoraji akionekana kwa pembeni anamchora, Wolper aliandika “ Ma Favorite tattoo place in Tz ..I love what he's doing” chini ya picho hiyo.
    Picha hii iliwafanya mashabiki wake wasubili kwa hamu kubwa kuiona tatoo hiyo mpya ya mwanadada huyu ambaye ni moja kati ya waigizaji wa hapa Bongo wenye wafuasi wengi huko mitandaoni.
    Zicheki picha zote hapo juu kisha funguka kwa jinsi ulivyoiona.

    Mfanyabiashara Wa Chips Atunukiwa Nishani Na Raisi Kikwete

    posted 4 hours ago by admin
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete juzi, ametunuku Nishani ya Ushupavu kwa mfanyabiashara ya kukaanga na kuuza viazi (chips) wa Dare s Salaam , Bwana Kassim Saidi Kassim, kwa kitendo chake cha kuokoa wananchi dhidi ya jambazi.
    Bwana Kassim Saidi Kassim alikuwa mmoja wa watunukiwa 28 wa nishani mbali mbali ambazo Rais Kikwete alitunuku ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 53 ya Uhuru.
    Katika sherehe ya kutunuku nishani iliyofanyika kwenye Bustani za Ikulu, Rais Kikwete alieleza kuwa amemtunuku Bwana Kassim Nishani hiyo kwa sababu ya kitendo cha ushupavu alichokionyesha cha kujitoa mhanga kukabiliana na jambazi mwenye silaha ambaye angeleta madhara makubwa.
    Katika maelezo yaliyosomwa kabla ya Rais Kikwete kumtunuku Nishani hiyo, ilielezwa kuwa mnamo Julai 7, mwaka jana, 2013, majira ya saa 3:15 usiku, Bwana Kassim akiwa katika eneo lake la biashara, alitokea jambazi akiwa na silaha aina ya bastola na kuanza kuwashambulia wateja kwa kuwapiga makofi na kuwapora mali zao na fedha zao.
    Na   “Kwa ushupavu mkubwa ulichukua chepe na kumpiga jambazi huyo mara mbili kichwani, kipigo kilichosababisha aanguke na kupoteza fahamu. Kitendo hicho kilifanikisha kukamatwa kwa bastola aina ya Globe ambayo nambari zake zilikuwa zimefutwa ikiwa na risasi tano ndani yake na hivyo kuepusha madhara ambayo yangeweza kusababishwa na matumizi mabaya ya silaha hiyo.”
    Bwana Kassim anakuwa muuza chips wa kwanza katika historia ya Tanzania kutunukiwa Nishani ya Ushapavu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    Bwana Kassim mwenye umri wa miaka 28 alizaliwa katika Kijiji cha Namwinyu, Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma mwaka 1986. Alisoma na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 2002 katika Shule ya Msingi ya Ilala, iliyoko Wilaya ya Ilala, Dar Es Salaam.
    Baada ya kumaliza elimu ya msingi, alianza kujishughulisha na biashara ya kukaaga na kuuza viazi(chips) katika eneo la Buguruni Malapa.

    Tuesday, December 9, 2014

    LULU: Bata la Watu Wa Bukoba Ni Noumer…Naendelea Kuoga Hela

    LULU: Bata la Watu Wa Bukoba Ni Noumer…Naendelea Kuoga Hela
    • LULU: Bata la Watu Wa Bukoba Ni Noumer…Naendelea Kuoga Hela 1
    • LULU: Bata la Watu Wa Bukoba Ni Noumer…Naendelea Kuoga Hela 2
    • LULU: Bata la Watu Wa Bukoba Ni Noumer…Naendelea Kuoga Hela 3
    • LULU: Bata la Watu Wa Bukoba Ni Noumer…Naendelea Kuoga Hela 4
     
    Mwigizaji wa filamu,mrembo na mwenye mvuto wa kufanya wengi wapagawe, Elizabeth Michael aka Lulu ambae kwasasa yupo Mjini Bukoba kwa mapumziko mafupi. Akiwa katika viwanja vya kula bata mjini hapo Lulu hakusita kuwasifia watu wa kabira la Wahaya kwa njinsi alivyo furahia GOOD TIME alilopewa na kumfanya afunguke mwenyewe kwenye mitandao ya kijamii
     “Wahaya noma......
    Hili Bata la Watu wa Bukoba ni Noumer...! likizo isiishe jamani
    Haikuishiahapo, alitupia picha nyingi mtandaoni akiwa "SAMUWEA" kama unavyoziona hapo juu. Lakini hiyo picha  ya miguu ndio iliua wengi, kwakuitendea haki alifunguka.
    “Nishawahi kusema naipenda miguu yangu!????
    Wallah Naipenda kwa Moyo mmoja ,oky naendelea kuoga hela..kuoga Maji mwisho Dar Es Salaaam...kwa kina Mutashobya(BUKOBA) ni kuoga Hela tu...!oky bye” Lulu alimaliza.
    Picha zote hapo juu. Bongomovies.com inamtakia likizo njema na arejee Dar es salaam salama.

    Monday, December 8, 2014

    Staa huyu hakusubiri kupewa zawadi ya Xmas kutoka kwa mtu yoyote, kajinunulia mwenyewe zawadi hii….

    images (3)Tuko kwenye mwezi ambao una Sikukuu nyingi na kubwa katika mwaka, ikiwemo ile ya tarehe 25 ambayo ni Sikukuu ya Christmas.
    Wengi tumezoea kupewa zawadi, lakini kumbe zawadi sio lazima kupewa hata wewe mwenyewe unaweza kujipa zawadi.
    Msanii kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke a.k.a Davido ameweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha zawadi ambayo amejinunulia kwa ajili ya Christmas ya mwaka huu na kuwashukuru mashabiki wake waliomsapoti Duniani kote.
    Amejinunulia gari aina ya Range Rover na kuweka picha ya gari hiyo ikiwa na maneno haya; “EARLY CHRISTMAS PRESENT FOR MYSELF!! BEEN A GREAT YEAR THANKS FOR ALL THE SUPPORT WORLDWIDE! I WOULDNT HAVE GONE THIS FAR WITHOUT U GUYS!!
    DavidoDavido II
    Hakika utapata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

    Monday, December 1, 2014

    Kama hujasoma Magazeti ya Leo Desemba 01 nimekuwekea hapa zile story kubwa zote.

    news
    MWANANCHI
    Diwani Hassan Kijuu alijikuta akiondolewa katika kikao cha Mkuu wa Mkoa na Watendaji wa Halmashauri, Diwani huyo akisema kwamba Mkuu wa Mkoa ameanza vibaya na kumtuhumu kuwa amekuwa akiwatisha Watendaji.
    Amri ya kuondolewa Diwani hiyo kutoka katika kikao hicho ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo baada ya kurushiana maneno ambapo Diwani huyo alipewa nafasi ya kuzungumza  kuhusiana na hatua ya ujenzi wa Maabara ilipofikia na Diwani huyo akaanza kwa kumlalamikia Mkuu huyo wa Mkoa kwamba hawezi kuzungumza habari za ujenzi wa Maabara wakati hajawaletea fedha.
    Mulongo amewataka Watendaji hao kutoa taarifa juu ya upotevu wa Bil. 40 katika Halmashauri hiyo kama ambavyo imeonekana kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG kuhusiana na upotevu huo.
    MWANANCHI
    Kituo cha afya Wilaya ya Bunda, Mara kiko katika wakati mgumu ambapo kituo hicho wameshindwa kutoa pesa Benki kiasi cha Sh. 3,139,590/- kutokana na wangehusika wote ambao walitakiwa kutia saini kuwa wamefariki, japo Diwani wa Kata ya Bunda amesema kuwa kiasi hicho cha pesa ni kidogo ukilinganishwa na hali ya uhitaji iliyopo.
    Mganga Mkuu wa Kituo hicho Charles Mkomba amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa litamalizika karibuni, kituo hicho kinategemewa na watu zaidi ya 120,000.
    MWANANCHI
    Wananchi wa Shinyanga wameshauriwa kuacha tabia ya kumaliza kesi za kikatili wa kijinsia kienyeji na kupelekea wahusika wa matukio hayo kutochukuliwa hatua za kisheria
    Hayo yamesemwa na Rachel Madundo ambaye ni mraghibishi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa katika Wilaya hiyo kwenye maadhimisho ya 16 ya siku ya kupinga ukatili wa kijinsia.
    Aidha amesema kuwa sababu inayopelekea kesi hizo kumalizwa kinyemela ni kutokana na kupewa rushwa huku idadi ya kesi zilizowahi kuripotiwa kuanzia Januari mpaka Oktoba kuwa ni nne tu kati ya 50 zinazohusu ukatili wa kijinsia.
    TANZANIA DAIMA
    Ajali mbaya imetokea Tanga ambapo watu saba wamefariki na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya Mitsubishi Canter yenye namba T 783 BLM majira ya saa 11:00 jioni siku ya jana.
    Kamanda wa Polisi Tanga Fressar Kashai alisema gari hilo lilitokea kijiji cha Ambangulu kwenye sherehe ya harusi na kupinduka likiwa njiani, chanzo chake hakijafahamika na dereva wa gari hilo Ramadhan Omar anashikiliwa na Polisi.
    NIPASHE
    Baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha maazimio kadhaa mwisho wa wiki iliyopita, imeonekana kwamba mzigo uliobaki sasa hivi ni kwamba Rais Kikwete ameachiwa kama mtu wa mwisho kufanya maamuzi juu ya azimio hilo.
    Bunge lilipitisha maazimio manane ikiwemo la kutenguliwa nyadhifa za Waziri wa Nishati na Madinii, Prof. Muhongo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema, Wanakamati wa Kudumu za Bunge hilo William Ngeleja (Sheria katiba na utawala), Andrew Chenge (Bajeti), na Victor Mwambalasa.
    Baada ya kamati kufanya maamuzi yake kazi imebaki kwa Rais Kikwete kufanya maamuzi.