Saturday, December 3, 2016
Saturday, November 7, 2015
Shuhuda aeleza jinsi Rais JPM alivyoingia Wizara ya fedha…..
By
Newsroom AlphaMsigwa House
Newsroom AlphaMsigwa House
on

Ni siku moja baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa kiti cha Urais ameanza kazi yake kwa surprise, Rais JPM amekatisha kwa mguu kutoka Ikulu mpaka Wizara wa Fedha maeneo ya Posta na kukuta ndani ya Ofisi kuna wafanyakazi ambao hawapo Ofisini na ilikuwa ni muda wa kazi.
ripota wa millardayo.com alikutana na
shuhuda akielezea namna alivyotembelea kutoka Ikulu mpaka kuingia Wizara
ya fedha..’Mimi niliona watu walikuwa wanakimbia kumbe alikuwa ni rais
wa awamo ya tano ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe
Joseph Magufuli anatembea kutokea Ikulu akielekea Wizara ya Fedha au
hazina alikuwa na walinzi pamoja na magari yake yalikuwa yakitembelea’ –
Shuhuda
‘Baada ya kutoka wizara ya fedha basi
akaingia kwenye gari, mimi hii ni mara yangu ya kwanza kuona kiongozi
kama huyu ameapishwa jana na leo ameanza kufanya kazi basi atakuwa kweli
ni Rais wa tofauti kabisa’ – Shuhuda
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Shuhuda akieleza jinsi Rais JPM alivyoingia wizara ya Fedha
Masanja kwenye foleni ya Ubunge Ludewa.. ataacha Komedi? asipopita? viatu vya Marehemu?

Uchaguzi Mkuu Tanzania umekwisha na zile
headlines mfululizo kuhusu Siasa zimeanza kupungua pia, lakini
hazijaisha… YES !! Bado headlines zitaendelea kutufikia kwa sababu kuna
Majimbo ambayo Uchaguzi ulisogezwa mbele baada ya kutokea matatizo
mbalimbali ikiwemo Wagombea wake kufariki.
RIP Marehemu Deo Haule Filikunjombe… stori inagusa Jimbo lake sasahivi, ni Jimbo la Ludewa lililopo Mkoa wa Njombe.
Mchakato kwenye Jimbo hilo umeanza, kwa
upande wa CCM ndio kumeshika kasi yenyewe, kwenye majina ya waliotangaza
kuitaka nafasi ya Uwakilishi wa Ludewa ndani ya Jengo la Bunge Dodoma,
yuko pia mchekeshaji Emmanuel Mgaya a.k.a ‘Masanja Mkandamizaji’ wa Orijino Komedi.
Hii ndio sababu ya yeye kugombea Jimbo la Ludewa >>> “Kwanza
nina uhakika mimi ndio Mgombea pekee mwenye uwezo wa kuleta maendeleo…
nilikuwa na wazo la kugombea Ubunge lakini nilijipa muda kwanza“- Masanja Mkandamizaji.
Kwanini kagombea kupitia CCM na sio chama kingine >>> “Mimi
ni mwanachama wa CCM na nimeamua kugombea nafasi hii kwa kupitia chama
changu, nipo katika siasa tangu siku nyingi ingawa mwanzo sikujitokeza
kwa sababu aliyekuwepo alijitosheleza.. nilichukua kadi ya Uanachama wa
CCM tangu mwaka 2005.”- Masanja.
Ikitokea hajapita kwenye Ubunge Je? >>> “Nisipopita kugombea Ubunge wa Ludewa, nitampa support yule ambaye atapewa nafasi kugombea“
Orijino Komedi na Ubunge? Hapo vipi mtu wangu ? >>> “Orijino
Komedi ipo, mimi sio member wa kundi… mimi ni Mwanzilishi, haimaanishi
kwamba nitafanya kazi za Ubunge kwa saa 24 kila siku… maendeleo yatakuja
Ludewa lakini Alhamisi kama kawaida, ‘chakachuwa nichakachuweee’…
siwezi kuacha Komedi, mbona nilikuwa Mchungaji na sikuacha Komedi..
nitakuwa Mbunge, Komedi na Church…“
Wanaojiuliza kama atavaa viatu vya marehemu je? >>> “Naamini
ndani ya utawala wangu jimbo la Ludewa litakuwa Jimbo la mfano, kuna
wengi wanasema kama nitavaa viatu vya marehemu…! Mimi sijaja kuvaa viatu
vya marehemu, ila nitahakikisha maendeleo ya Ludewa yanakua kwa kasi.”-Hivyo ndio alivyomaliza Mchekeshaji anayewakilisha kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji na headlines zake kwenye Ubunge wa Ludewa.
Picha 7 za JK alivyoagwa Ikulu.. Rais JPM ofisini na ziara ya kushtukiza Wizarani..

Hizi picha ni mkusanyiko wa matukio makubwa matatu Tanzania leo November 6 2015… Rais John Pombe Magufuli tayari kaanza kazi !!
Naanza na pichaz za Rais Mstaafu JK alivyoagwa Ikulu kwenda Kijijini kwao Msoga, Chalinze.
Hapa ni picha moja ya Rais JPM siku ya kwanza Ofisini kwake, Ikulu Dar es Salaam.
Hapa ni picha kwenye ziara yake ya
ghafla aliyoifanya Wizara ya Fedha, Posta Dar es Salaam na kukuta baadhi
ya wafanyakazi hawapo.
Thursday, October 1, 2015
Hii mpya ya Chui kunasa kwenye chungu cha maji huko India isikupite…(Video)
By
Prince TZA
Prince TZA

Taarifa hiyo iliripotiwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo na kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ambapo katika video alionekana chuo huyo akijitahidi kujitoa lakini haikuwezekana hadi walipokuja maafisa wa wanyama pori.

Iliwachukua zaidi ya masaa sita kwa maofisa hao kuweza kufanikisha zoezi hilo la kumtoa kisha kumrejesha kwenye hifadhi yake.
Thursday, September 17, 2015
Mapenzi yake kwa Manchester City yamemfanya shabiki huyu wa Kihindi kuamua hivi..
By
Alpha Msigwa TZA
on

Mpira wa miguu ni mchezo ulioteka hisia za watu wengi katika soka hususani wanaume, imekuwa ni kitu cha kawaida kuona mtu akijichora rangi mwilini mwake kama ishara ya kushangilia timu yake. Hili linaweza kuwa geni kwa ukanda wa Afrika Mashariki lakini Ulaya imezidi kushika kasi.
Shabiki wa klabu ya Manchester City Suraj Nandurkar ameingia kwenye headlines ya vyombo vya habari baada ya kuamua kuchora tattoo ya majina ya wachezaji waManchester City anaowapenda Suraj Nandurkar. Licha ya kukosea spelling majina ya Aleksandar Kolarov na Fernandinho, shabiki huyo anakiri kugundua kosa baada ya kumaliza kuchora.
Suraj Nandurkar ambaye ana umri wa miaka 28 alianza kuipenda klabu ya Manchester City mwaka 2012 baada ya Sergio Aguero kufunga goli lililomvutia katika mechi dhidi yaQPR. Suraj Nandurkar anafanya kazi na kuishi kwao Mumbai India.
Monday, September 14, 2015
MICHEZO
Hiki ndicho kilichowakuta Espanyol walipocheza na Real Madrid leo
By
Alpha Msigwa
on

Ligi kuu ya Uhispania imeendelea leo baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa kumalizika, Real Madrid walisafiri mpaka jijini Barcelona kwenda kucheza na Espanyol.

Mchezo uliopigwa katika dimba la Cornella El Plat umeshuhudia mwanasoka anayeshikilia taji la uchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo akifunga magoli 5 katika mchezo uliomalizika kwa Real Madrid kushinda 6-0.
Subscribe to:
Posts (Atom)