MICHEZO
Hiki ndicho kilichowakuta Espanyol walipocheza na Real Madrid leo

Ligi kuu ya Uhispania imeendelea leo baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa kumalizika, Real Madrid walisafiri mpaka jijini Barcelona kwenda kucheza na Espanyol.

Mchezo uliopigwa katika dimba la Cornella El Plat umeshuhudia mwanasoka anayeshikilia taji la uchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo akifunga magoli 5 katika mchezo uliomalizika kwa Real Madrid kushinda 6-0.
No comments:
Post a Comment