Monday, November 17, 2014

MWANBUSI WA MBEYA CITY ANG'ATUKA!!


Ripoti kadhaa ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi amejiuzulu .
Hatua hiyo imekuja baada ya kuishuhudia timu yake ikipata mfululizo wa matokeo mabaya kwenye ligi ambapo katika michezo saba imeweza kushinda mchezo mmoja pekee huku ikitoka sare kwenye michezo miwili na kufungwa jumla ya michezo minne .
Taarifa mbalimbali toka jijini Mbeya zinasema kuwa kwa muda mrefu wachezaji wa Mbeya City walikuwa wamepoteza Imani na kocha wao hali ambayo mashabiki wanaamini kuwa imechangiwa na pengo la aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo Maka Mwalusi .

Mwalusi ambaye alihama Mbeya City na kwenda kuifundisha timu ya ligi daraja la kwanza ya Panoni Fc ya mjini Moshi anadaiwa kutoridhishwa na kitendo cha kupewa ‘mgao kiduchu’ wa zawadi ya kocha bora ambaye bosi wake Mwambusi aliipata hali ambayo ilionyesha kutothaminiwa kwa mchango wake .
Hali ya Juma Mwambusi ilikuwa inaonekana kuwa mbaya kadri Mbeya City ilivyozidi kupata matokeo mabaya hasa baada ya kujikuta ikipoteza michezo minne mfululizo mbele ya timu za Azam Fc , Mtibwa Sugar , Mgambo Jkt na Stand United.
Endapo taarifa hii itathibitika kuwa Kweli Mwambusi ambaye msimu uliopita alitwaa tuzo ya kocha bora wa msimu kabla ya kutwaa tuzo nyingine ya kocha bora wa mwezi septemba wakati ligi ilipoanza atakuwa kocha wa pili kupoteza kibarua chake baada ya Denis Kitambi ambaye alifukuzwa kazi na Ndanda Fc baada ya matokeo mabaya .

Friday, November 14, 2014

Taarifa kuhusu ajali nyingine ya moto Dar.

Huu ni mfano wa Gari la Kikosi cha Zimamoto.
Huu ni mfano wa Gari la Kikosi cha Zimamoto.
Taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita ni kuhusu tukio la ajali ya moto Dar es salaam.
Kupitia kipindi cha HIGHLANDS JAM kinachorushwa na HIGHLANDS FM,mtangazaji BENNY MBILINYI  ametoa taarifa kuhusiana na jali ya moto iliyotokea katika jengo la Machinga Complex lililopo Ilala, Dar es saalam
Chanzo cha moto huo mpaka sasa hakijafahamika na tunaendelea kufuatilia ili kukupa taarifa zaidi na hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo.
IMG-20141114-WA0003
IMG-20141114-WA0004 IMG-20141114-WA0005
Wananchi wakitazama jingo hilo linanyo teketea kwa moto
IMG-20141114-WA0008
Gari la Zima moto wakijalibu kuzima moto huo

Wednesday, November 12, 2014


#Breaking Rapper Geez Mabovu amefariki dunia usiku huu

Geez Mabovu
Geez Mabovu ni ambae hajavaa shati.
Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku November 11 2014.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam.
Geez Mabovu 2
Geez 3
Hii ni picha ya July 2013 ambayo ni mara ya mwisho Geez Mabovu ameonekana kwenye millardayo.com akiwa na Baba yake Dully Sykes maeneo ya Kinondoni Dar es salaam nje ya Bar ya msanii Dudubaya aliyokua ameifungua wakati huo.
Dennis ambae alikua mtu wa karibu wa Geez Mabovu amethibitisha 
pia
 kuhusu kifo cha Geez Mabovu na kusema rapper huyu aliondoka Dar kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya.
Kwa mujibu wa Denis, Geez atazikwa kesho jioni November 13 2014. #RIP

Tuesday, November 11, 2014

MAMBO 13 YA KUKUFANYA UFANIKIWE MAISHANI

Mbinu 13 na rahisi za kupata ujasiri ujasiri kimafanikio.
1. Kutoshindana na waliofanikiwa.

Daima mtu ahakikishe anawafanya waliofanikiwa wajione wapo juu. Kama mtu anataka kuwashangaza basi asionyeshe ujuzi wake wote. 
Kuwapa waliofanikiwa heshima yao kutamfanya mtu apate msaada na hatimaye afikie kiwango cha juu bila ya kupata tabu nyingi. 

Mfano, mtu asishindane na mwajiri wake ili kuonekana anajua sana; asishindane na tajiri katika matumizi hususani mazingira ya kijamii kama baa, misiba n.k. Waliofanikiwa hutafsiri kitendo cha kushindana kama kuonyesha kiburi au maskini jeuri.

2. Kutoamini sana marafiki.

Mtu awe makini 'anapojamiiana' na marafiki au watu wa karibu. Watu wa karibu huwa wasaliti na huvujisha siri kwa wapinzani. Mtu aogope marafiki zaidi ya maadui, ikibidi awape nafasi wale anaohisi ni wapinzani. Ilkiwa mtu hana wapinzani, ajitahidi kuwatafuta. Mtu ajifunze jinsi ya kutumia wapinzani kimafanikio, si kuwaamini marafiki muda wote.

3. Kuficha malengo.

Mtu afiche matarajio yake au dhamira za matendo yake. Kuweka malengo hadharani huwafanya watu wenye nia mbaya kujipanga na kuvuruga malengo husika. Mtu akinge malengo yake na ikiwa yatagundulika iwe nyakati za mwisho; nyakati ambazo wapinzani hawawezi kuweka vikwazo.

4. Kutumia wasidizi.

Kufankiwa kwa mtu kunategemea mchango anaoupata kutoka kwa wale wanaomzunguka (mazingira na marafiki). Mtu atumie busara, ujuzi na maarifa ya wale anaofanya nao kazi ili kusonga mbele. Msaada haupunguzi tu nguvu, bali 
pia
 huongeza ufanisi na kuimarisha urafiki. Mtu hupata fadhila kutoka kwa wasaidizi wake, ndipo jamii husika. Hivyo, mtu awaachie watu wengine yale wanayoweza kufanya kwa ufanisi.

5. Kushinda kupitia matendo.

Ushindi mtu anaopata kupitia maneno haufai kitu! Mtu asishindane juu ya uwezo wake kwa maneno bali, aache matendo yaongee. Ushindi makini ni ule mtu anaoupata kupitia matendo yake, na si kwa wingi wa maneno. Uhalisia wa matendo huonyesha umakini wa mtu kwa jamii inayomzunguika. Mtu husifiwa kwa kadiri ya juhudi zake za hali na mali kutatua changamoto zinazomsonga, si kwa kupiga domo.

6. Kujenga utegemezi.

Ili mtu kujua umuhimu wake katika jamii anapswa kjua kwa kiasi gani mchango wake unahitajika. Mtu ajenge mazingira ya kutegemewa; kutegemewa kuleta furaha au ustawi katika mazingira yanayomzunguka. 

Ili kfanya hivyo, mtu asitoe mbinu zote alizo nazo juu ya kitu fulani. Kutegemewa humwezesha mtu 'kuuza' kile alichonacho kwa mafanikio yake na ya jamii yake. Hivyo, mtu ajue wakatigani wa kuficha huduma yake, wakati gani wa ktoa kidogo na wakati gani wa kutaka watu wailipie.

7. kutenda kama mpelelezi.

Ni muhimu sana mtu kujua juu ya wapinzani wake. Mtu atumie marafiki (wapambe) ili kupata taarifa muhimu juu ya udhaifu na uwezo wa wapinzani wake. Kufanya hivyo kutamwezesha mtu kupanga mipango ya kiulinzi na ambayo haitazimika katika safari yake ya mafanikio. Kupata taarifa kunafanikishwa kwa kuuliza maswali rahisi, kuuliza kwa njia ya upole na kwa kutumia mifano. Kila wakati ni fasaha kwa upelelezi.

8. Kuwafahamu watu wa karibu.

katika mazingira yoyote yale kuna watu wa aina nyingi. Watu hutofautiana kiimani, kitabia, kimalengo, kiutendaji n.k. Watu wa karibu ndio wanaotoa au kufanikisha kotoa ushindani katika mazingira yasiyotegemewa. Watu wengi, tena wa karibu ni kama mbwa mwitu. Ili kufahamu watu wa karibu, mtu atafakari kwa kina misingi mikuu ya urafiki huku akibadilisha muonekano, kutoa changamoto kwa walengwa n.k. Pindi mtu anapofanya yote hayo atazame mwitikio ya walengwa.

9. Kuwa na dira.

Dira humwezesha mtu kufika kule anakotaka. Mtu anapaswa kuweka malengo juu ya kule anakotaka kufika baada ya muda fulani pia, changamoto azazohisi zitamkumba sambamba na suluhu sahihi. Kwa kuwa na malengo haitakuwa ngumu sana kukabiliana na vikwazo mtu awapo safarini. Watu wengi huweka malengo huku wakisahau au kupuuzia adha zinazoweza kuwakumba au zilizowakumba watu wengine waliokuwa na malengo kama yao.

10. Kujikuza.

Mtu asipokee na kukubali sifa 'chafu' anazopewa na jamii. Mtu anapaswa kujikuza kwa kuvaa utambulisho mpya; ambao unavuta umakini na hauiudhi jamii yake. Mtu anapaswa kutawala taswira yale, si taswira yake ktawaliwa na nguvu kutoka nje. Kujikiza kwa jitihada za mtu huleta taswira ya kudumu, na ambayo italeta uaminifu wa kweli na kukubalika katika jamii.

11. kuwa na shabaha.

Mtu anapaswa kuelekeza nguvu na jitihada kwa yale anayoamini yataleta matunda mazuri. Mtu awe makini kutunza au kutenga nguvu za ziada kwa ajili ya changamoto. Ili kutokata tamaa, mtu anapswa kuwa na wadu (watu wa karibu) wenye uwazo tofauti tafauti kama vile madaktari, wafanya biashara, waalimu, viongozi wa dini, wazee wenye busara n.k

12. Kujirudisha nyuma.

Kama mtu akiona changamoto zitamzidi siku a usoni, huku mbinu alizo nazo au mikakati yake itakuwa dhaifu ahairishe 'pambano'. Kurudi nyuma kutampa mtu nafasi ya kujipanga kwa kukusanya nguvu na 'kuusoma mchezo zaidi'. Mtu asikubali kuangushwa kabisa na changamoto ndipo ajiandae kuinuka. Ni vigumu sana mtu kuamka baada ya kushambuliwa na kuangamizwa na chahangamoto za kimaisha.

13. Kutojitenga.

Kujitenga na jamii au marafiki ni hatari sana! Kwani ulimwengu ni tambara bovu na uumejaa wapinzani kila kona. Inapasa mtu kujiundia ngome ya ulinzi lakini, si kwa kujitenga. Kujitenga hupunguza mawasiliano na watu na pia uwezekano wa kupata misaada ya hali na mali. Kwa mfano, kuna uwezekano mkubwa wa kukosa habari, ushauri, vitendea kazi n.k. Vitu ambavyo ni muhimu kufikia mafanikio. 

TAZAMA PICHA NYMBA ALIYOKUWA AKIISHI BABU WA LOLIONDO NA NYUMBA YAKE YA HIVI SASA, NI SHIDAAH

   
Hii ni nyumba aliyokuwa anaishi Babu Ambi kabla Dozi ya Kikombe haijachangany

FILAMU YA MWISHO KUFANYWA NA MAREHEMU SHALO MILIONEA.

MBUNGE AANGUKA GHAFLA BUNGENI DODOMA, AKIMBIZWA HOSPITALINI..NI HUYU HAPA

Mbunge wa Mbeya Vijijini Mh.Mchungaji Luckson Mwanjale akiwa amebebwa na wahudumu wa afya baada ya kudondoka ndani ya Jengo la Ukumbi wa Bunge jana mchana.
Chanzo cha kuanguka kwake huko bado hakijafahamika na sasa yuko kwenye uangalizi wa madaktari kwa uchunguzi zaidi.

 
SOMA HAPA ALICHOANDIKA HEMEDY PHD KUHUSU MSANII WA TANZANIA ALIESEMA HAFANYI TENA COLLABO NA WABONGO.
Screen Shot 2014-11-10 at 11.03.32 AMMwigizaji/Mwimbaji Hemedy PHD ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao hutumia sehemu ya muda wao pia kuandika kwenye mitandao ya kijamii yake ya moyoni ama kuwafikishia taarifa mashabiki wake.
November 10 2014 Hemedy aliandika tweet ikisema >>> ‘Mtu anasema hategemei kufanya collabo na msanii wa bongo ikiwa ngoma zake zote kabebwa na collabo, fikiri kabla ya kuzungumza‘
Hemedy ameandika tweet hii siku kadhaa baada ya msanii Shetta kusema kwa sasa hafikirii kufanya collabo na Wasanii wa Tanzania bali anafanya mpango wa kujipenyeza kimataifa zaidi akisema ‘nimefanya collabo nyingi na Wasanii wa Tanzania ndio maana siko tayari kufanya tena hivyo nikawa nawaza mawili, nifanye collabo na msanii wa kimataifa au kutoa wimbo peke yangu?

Monday, November 10, 2014

MAKAMUZI YA NGUVU KATIKA USIKU WA ZAX 4 REAL JIJINI MBEYA BIG UP ONE DAY YAS Story by PRINCE ALPHA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya afahamikae kwa jina la Zax 4 Real, Anae fanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya jijini mbeya, Amefanya vizuri pia katika show yake ya Usiku Wa Zax 4 Real, iliyo dhaminiwa na vituo vya redio vya Mbeya Fm, Bomba Fm,Rock Fm,G.Fm,Highlands Fm,Sweet Fm,Boys 2 Men Fasheni,Southside Music,Cigger Foundation na Michuzi Media Group. Katika ukumbi wa Nebana pub Soweto jijini Mbeya.Picha na Mr. Pengo wa Globu ya Jamii,Mbeya.
Msanii Zax 4 Real akiwapagawisha mashabiki wake ndani ya NEBANA PUB
mwana dada Silvia Green Kutoka jijini mbeya,akikamua katika stage ya Usiku wa zax 4 Real.
kijana anae kimbiza katika muziki wa kizazi kipya Davy Star akifanya makamuzi katika show hiyo. 

Sunday, November 9, 2014

Umri wamvua Miss Tanzania taji

  • 10 Novemba 2014
null
Miss Tanzania Sitti Mtemvu amejivua taji la Miss Tanzania aliloshinda mwaka huu mjini Dar es Salaam baada ya kuzongwa na mashabiki kuhusu umri wake.
Akizungumza na BBC Mkurugenzi wa Lino International Agency Hashim Lundenga waandaji wa shindano la Miss Tanzania amesema kuwa mrembo huyo amejivua mwenyewe taji hilo kwa kuandika barua bila kushinikizwa na mtu yeyote.
Tangu atangazwe mshindi kumekua na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu wakimtuhumu kuwa alidangaya umri wake ili atimize vigezo vya kushiriki shindano hilo.
Pia Sitti alituhumiwa kuwa ana mtoto jambo ambalo pamoja na shutuma zingine alikanusha mbele ya waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.
Kamati hiyo imemtangaza Lilian Kamazima ambaye ni mshindi namba mbili wa Miss Tanzania

Tuesday, November 4, 2014

RATCO Waleta Mabasi ya Hali ya Juu Kiteknolojia

Sambaza Teknokona
 

ratco2Kampuni ya mabasi ya Ratco imeamua kujitutumua kiukweli kwa kuleta mabasi ya kipekee zaidi kiteknolojia kutoka kampuni ya mabasi ya China ya Yutong, inasemekana mabasi hayo mapya yatakuwa yafanya ruti ya Dar -Tanga. Na kwa eneo la VIP utaweza kukaa kwenye siti za ubora wa hali ya juu na hii ikiwa ni pamoja na skrini ya TV/tableti mbele yako kukuwezesha kuangalia video au kusikiliza muziki – kama kwenye ndege vile.


Tazama picha za basi hilo hapa;
ratco1 ratco3 ratco4