Tuesday, April 22, 2014

Picha ya producer C9 baada ya kupata ajali na kuumia kichwani

c9 - CopyHuyu ni producer maarufu na ametengeneza  nyimbo kama Mama Ntilie ya A.T na nyimbo nyingi za marehemu Sharo milionea. Hivi sasa anawania tuzo ya KTMA kwenye kipengele cha mtayarishaji bora wa muziki wa bendi na hivi karibuni amepata ajali ya bajaj na kuumia kichwani

Sikiliza You heard inayomhusu Chid Benz kumpiga msichana siku ya Pasaka.

Inasemekana April 20 Mwanadada Aisha Sued ambaye ni mkazi wa Ilala karibu na Kituo cha basi Msaada Garage amedai alishambuliwa na Chidi Benz na kuumizwa vibaya mdomoni hadi kushonwa nyuzi 18.

Tukio hilo ambalo inasemekana lilitokea moja kati ya Bar zilizopo Ilala usiku wa sikukuu ya Pasaka taarifa zilizopo toka usiku wa Pasaka mpaka sasa hivi Chidi Benz yupo chini ya Jeshi la Polisi kituo cha polisi Pangani Ilala kwa madai ya Shambulio na kumuumiza vibaya Aisha Sued.

chidImage00001

Baada ya kutangaza kumfukuza Moyes,huyu ndiye kocha mpya aliyepokea mikoba yake..

giggsKutokana na kutofanya vizuri chini ya uongozi wake David Moyes hatimaye leo April 22 Manchester United wamemtangaza Mchezaji wa siku nyingi wa Manchester United Ryan Giggs kukabidhiwa  kwa muda mikoba ya David Moyes aliyetimuliwa kazi leo

Saturday, April 19, 2014

Marehemu Gurumo kwa maisha yake yote alikuwa na ulemavu wa jicho moja lakini hakuna mwanamuziki wala mdau  au mwanahabari aliyekuwa anajua sababu ya madhila hayo ya mzee wetu mpendwa.


Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.

Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.

“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.
Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.

“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akiwa na jicho lake.

Hii ya Waumini kusafisha barabara ya Lami kwa sabuni kama hivi umeipata?Screen Shot 2014-04-20 at 1.08.01 AMRipota wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoitch anaripoti kwamba wakazi wa jiji la Eldoret wamemfanya kila alieiona hii kuvutiwa na pengine kujua imekuaje wakafanya hivi kwa mara ya kwanza baada ya kujitosa na kupiga deki barabara ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya.

Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya kumlaki nabii Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya leo na siku ya Jumatatu kuadhimisha pasaka na kumshukuru jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret kufanyika uchaguzi wa amani mwaka 2013
Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii maoni yalikotolewa na Wakenya kuhusu hii ishu, maoni mengi yameonekana kupinga kitendo cha waumini hao wa kanisa la Jesus is lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima kupita kiasi.
Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki Radio ya kass fm inayotangaza kwa lugha ya kikalenjin inayozungumzwa na wakazi wa jiji la Eldoret Julius lamaon, amesema ‘watu wetu waache kupotoka, jiji letu limebadilishwa na kuwa jiji la vituko…… Gavana hatakiwi kuhudhuria mkutano huu’