
Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.
Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.
“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.
“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akiwa na jicho lake.
No comments:
Post a Comment