Hii ya Waumini kusafisha barabara ya Lami kwa sabuni kama hivi umeipata?
Ripota wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoitch anaripoti kwamba
wakazi wa jiji la Eldoret wamemfanya kila alieiona hii kuvutiwa na
pengine kujua imekuaje wakafanya hivi kwa mara ya kwanza baada ya
kujitosa na kupiga deki barabara ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret
kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya.
Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya kumlaki
nabii Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya leo na siku ya Jumatatu
kuadhimisha pasaka na kumshukuru jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret
kufanyika uchaguzi wa amani mwaka 2013
Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii maoni yalikotolewa
na Wakenya kuhusu hii ishu, maoni mengi yameonekana kupinga kitendo cha
waumini hao wa kanisa la Jesus is lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima
kupita kiasi.Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki Radio ya kass fm inayotangaza kwa lugha ya kikalenjin inayozungumzwa na wakazi wa jiji la Eldoret Julius lamaon, amesema ‘watu wetu waache kupotoka, jiji letu limebadilishwa na kuwa jiji la vituko…… Gavana hatakiwi kuhudhuria mkutano huu’
No comments:
Post a Comment