Sikiliza You heard inayomhusu Chid Benz kumpiga msichana siku ya Pasaka.
Inasemekana April 20 Mwanadada Aisha Sued ambaye ni mkazi wa Ilala
karibu na Kituo cha basi Msaada Garage amedai alishambuliwa na Chidi
Benz na kuumizwa vibaya mdomoni hadi kushonwa nyuzi 18.
Tukio hilo ambalo inasemekana lilitokea moja kati ya Bar zilizopo
Ilala usiku wa sikukuu ya Pasaka taarifa zilizopo toka usiku wa Pasaka
mpaka sasa hivi Chidi Benz yupo chini ya Jeshi la Polisi kituo cha
polisi Pangani Ilala kwa madai ya Shambulio na kumuumiza vibaya Aisha
Sued.


No comments:
Post a Comment