- Unajua kuna nchi zinapiga marufuku watoto kupewa baadhi ya majina? Yako hapa...
Unajua kuna nchi zinapiga marufuku watoto kupewa baadhi ya majina? Yako hapa…

Huku kwetu tuna utaratibu wa kuwapa watoto wetu majina tunayopenda, yapo majina ya watu maarufu kama viongozi, wanasoka, waigizaji na wengineo.
Kuna hizi nchi ambacho wao wamepiga marufuku baadhi ya majina kupewa watoto, list ni hii hapa.
New Zealand: Msajili wa Vizazi, Vifo na Ndoa nchi hii ameagiza baadhi ya majina kupigwa marufuku ikiwemo majina haya; Majesty, Queen Victoria, Lucifer na jina la Mafia No Fear.
Venezuela: Wao wamezuia matumizi ya jina la Superman kwa kuwa ni gumu kulitamka.
Denmark: Wametoa list ya majina rasmi ambayo yako zaidi ya 7,000 mtoto akizaliwa anachaguliwa jina kati ya majina hayo, moja ya majina yaliyozuiwa huku ni jina la Monkey.
Brazil: Jina lililozuiwa huku ni jina la Saddam Hussein.
Mexico: Wamepiga marufuku mtoto kupewa majina ya Scrotum, Terminator, Burger King, Hitler na Virgin.
Uturuki: Mahakama imezuia mtoto kupewa jina la Osama Bin Laden
Portugal: Wao wamezuia jina la Tom.
Mfano hii ingekuja Bongo, majina gani ungependa yazuiwe wasipewe watoto wetu?
Previous post link Stori 8 zilizopewa headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 30, 2015, nimekuwekea hapa
Next post linkUpo Dar na ungependa kwenda cinema leo? ratiba iko hapa