Tuesday, January 20, 2015

Nimerekodi Hekaheka ya leo Jan 20, inahusu msichana wa kazi aliyelalamika kunyanyaswa



Hands
Kama ulipitwa na  Hekaheka ya leo January 20 inatokea Dar, msichana mmoja aliyekuwa akifanya kazi za ndani alifika ofisi za Clouds FM akilalamikia kuteswa na bosi wake na kumtishia kumchoma kisu, alipoomba nauli ili arudi kwao bosi wake alikataa.
Msichana huyo alitoroka na kuanza kuomba msaada ili aweze kupata shilingi elfu 60 kama nauli ya kurudi kwao.
Bosi wake alipofuatwa alikiri kuwa msichana huyo alikuwa mfanyakazi wake, ameishi naye kwa muda mfupi  lakini alisitisha mkataba naye kutokana na binti huyo kuwa na ujauzito aliokuja nao kutoka Kigoma na ishu hiyo ilishafika hadi kituo cha Polisi.
Bonyeza play kuisikiliza Hekaheka hiyo hapa.

No comments:

Post a Comment