Tuesday, January 27, 2015

HALI inazidi kuwa mbaya kwa mastaa wawili wa muziki wa Bongo Fleva wanaogombea unyota kimuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, safari hii yameibuka mapya kwa kila msanii kuogopa kumshika mkono mwenzake kutokana na imani za kishirikina.

Mashabiki wa Mbongofleva Ali kiba waliionyesha kumkubali zaidi kuliko, 'Daimond Platnumz' katika viwanja vya Leaders Club.

TUJIUNGE LEADERS 
Matukio hayo ya kusisimua yaliwatia hofu kubwa mashabiki na wadau wa muziki Bongo muda mfupi kabla ya nyota hao kukaribishwa stejini kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita.

HIRIZI ZAKUTWA UWANJANI
Kwa mujibu wa wanahabari wetu, katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni, kulikutwa hirizi zilizozagaa, zilizodaiwa kudondoshwa  na vijana waliokamatwa wakiwa wamevalia sare zenye majina ya mastaa hao wawili.


No comments:

Post a Comment