Mapenzi yake kwa Manchester City yamemfanya shabiki huyu wa Kihindi kuamua hivi..

Mpira wa miguu ni mchezo ulioteka hisia za watu wengi katika soka hususani wanaume, imekuwa ni kitu cha kawaida kuona mtu akijichora rangi mwilini mwake kama ishara ya kushangilia timu yake. Hili linaweza kuwa geni kwa ukanda wa Afrika Mashariki lakini Ulaya imezidi kushika kasi.
Shabiki wa klabu ya Manchester City Suraj Nandurkar ameingia kwenye headlines ya vyombo vya habari baada ya kuamua kuchora tattoo ya majina ya wachezaji waManchester City anaowapenda Suraj Nandurkar. Licha ya kukosea spelling majina ya Aleksandar Kolarov na Fernandinho, shabiki huyo anakiri kugundua kosa baada ya kumaliza kuchora.
Suraj Nandurkar ambaye ana umri wa miaka 28 alianza kuipenda klabu ya Manchester City mwaka 2012 baada ya Sergio Aguero kufunga goli lililomvutia katika mechi dhidi yaQPR. Suraj Nandurkar anafanya kazi na kuishi kwao Mumbai India.