Sunday, March 30, 2014


MAPEMA wiki iliyopita uvumi ulisambaa nchini England kwamba gazeti maarufu la The Sun lilikuwa mbioni kuchapisha stori ndefu iliyohusu kashfa ya ushoga ya mlinzi mmoja wa sasa wa kushoto wa timu ya taifa ya England.


Hata hivyo, Gazeti la The Sun la juzi Jumapili lilikanusha kutaka kuandika stori hiyo, lakini bado mlinzi wa kushoto wa England na Chelsea, Ashley Cole akawahi kukanusha kwamba alikuwa hahusiki na kashfa hiyo.

Cole ameimiliki nafasi ya ulinzi upande wa kushoto tangu Machi 2001 na ndiye mchezaji wa pembeni aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha timu ya taifa ya England.

Na kama kutakuwa na ukwlei wowote katika habari hiyo ni wazi kwamba hilo litakuwa pigo jingine kwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anahaha kupata namba hiyo hiyo aliyoitawala muda mrefu katika kikosi cha Chelsea na hivyo hiyo kuwa nuksi nyingine inayomuandama mchezaji huyo.

Mashabiki wengi waliamini kwamba Cole alikuwa anahusika na kashfa hiyo.

Mwingine aliyeonekana kuhisiwa katika kashfa hiyo ni mlinzi kinda, Luke Shaw ambaye ameanza kuichezea timu ya taifa ya England katika pambano la kirafiki dhidi ya Denmark Machi 8 mwaka huu. Hata hivyo wote wawili wametumia mitandao yao ya mawasiliano kukanusha uwepo wa habari hiyo.

Cole aliandika katika mtandao wake akisema ‘strictly chicks only’, akimaanisha anapenda wasichana tu, wakati Shaw aliandika kwa kusema ‘Si mimi’. Cole alikuwa katika ndoa na mwanamuziki maarufu wa Kundi la Girls Aloud, Cheryl Cole ambaye pia aliwahi kuwa jaji wa michuano ya kusaka vipaji ya X Factor lakini ndoa yao ikavunjika mwaka 2010 kutokana na kile kilichodaiwa kuwa Cole hakuwa mwaminifu katika ndoa hiyo.

Uvumi ulitanda Jumamosi usiku iliyopita katika mitandao ya kijamii kwamba The Sun la Jumapili lingemtaja mchezaji mmoja katika kikosi cha kocha Roy Hodgson ambaye anahusika na kashfa ya ushoga.

Kama gazeti hilo lingefanya hivyo, huyo angekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya timu ya taifa ya England kujitangaza kuwa shoga. Hata hivyo gazeti hilo lilikanusha waziwazi kwamba stori hiyo ilikuwa imepikwa na watu wasiojulikana.

Huo ni mwendelezo wa habari za ushoga zikuibuka katika vyombo vya habari vya Uingereza baada ya staa wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Thomas Hitzlspelger kujitangaza kuwa shoga Januari mwaka huu.

Nyota huyo wa zamani wa Aston Villa, Everton na West Ham amekuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu England katika mfumo mpya kujitangaza kuwa shoga.

  Kala Jeremiah azungumzia kutochaguliwa kuwania KTMA mwaka huu licha ya kushinda tuzo nyingi mwaka jana

Mshindi wa tuzo kadhaa za muziki za Tanzania (KTMA 2013), Kala Jeremiah ambaye mwaka huu jina lake halikutajwa katika vipengele vyote vya kuwania tuzo hizo ametoa mtazamo wake kuhusu kutotajwa kwake.

Rapper huyo wa Rock City Mwanza amesema kuwa moyo wake uko sawa na anaona kila kitu kiko sawa na kwamba hana hata swali.
“Yaani mimi sijui nikoje, nimezaliwa tofauti sana nadhani na binadamu wengine. Yaani ni mtu fulani wa ajabu sana, naonaga kila kitu kiko sawa. Moyo wangu uko tofauti sana, sina tatizo lolote yaani sijui nikwambieje…yaani niko very comfortable na naona ni sawa kabisa sina swali sina chochote kwenye moyo wangu niko vizuri. Naona ni Mungu aliniumba vizuri sana hivi nilivyo kwa sababu kila kitu nakichukulia fresh.” Kala Jeremiah aliniambia Tovuti ya Times Fm.
Ameeleza kuwa anaona watu walioingia walistahili kuingia na kwamba hata mwaka jana hakuwa anatarajia kuingia kwenye vipengele hivyo na hata kushinda, kwa hiyo hata mwaka huu pia alikuwa hatarajii chochote.
“Ndio maana nilipotajwa mwaka jana nikashtuka na hata nilipopata tuzo pia nikashtuka. Yaani kila kitu mi nadhani kinatakiwa kije chenyewe kwa sababu ukikifikiria kitu…mi naona hata kukifikiria kitu na kupanga eti itakuwa hivi au itakuwa hivi, no. Sidhani kama hiyo ni njia sahihi, njia sahihi mimi naona ni kufanya kazi nzuri na kuacha watu wafurahi na kazi zako.” Ameongeza rapper huyo wa Wale Wale.
Kala ameeleza kuwa hata wakati anashiriki mashindano ya BSS hakuwa na wasiwasi wa kuendelea ama kutoendelea na mashindano kwa kuwa kwake yeye huona kila kinachotokea katika hali hiyo ni sawa.
Wimbo wa Dear God uliotayarishwa na Dee Classic ulimpa tuzo tatu muhimu mwaka jana ikiwa ni pamoja na tuzo kubwa ya wimbo bora wa mwaka. Alishinda pia tuzo ya msanii bora wa hip hop akiwabwaga Fid Q, Joh Makini, Profesa Jay na Stamina.
Kala aliitoa tuzo ya wimbo bora wa hip hop na kumkabidhi mama yake Albert Mangwea kwa heshima na kumuenzi rapper huyo aliyefariki May 28 mwaka jana nchini Afrika Kusini.

(Photo’s) The Making Of Music Video NITAFURAHI kutoka kwa NEYCOMS

IMG-20140329-WA0011 

Ni msanii mchanga katika game hili la Bongo Fleva na jina lake la kisanii anaitwa NEYCOMS anatarajia kuachia video yake mpya aliyoipa jina la NITAFURAHI ikiwa imesimamiwa na kampuni ya URBAN VIDEOS na hizi ndio baadhi ya picha zilizopigwa wakati wakishoot video hiyo.

 

IMG-20140329-WA0012

 IMG-20140329-WA0016

Wednesday, March 26, 2014

BABA AMNYONGA MWANAE MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA KISHA KUACHA UJUMBE TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI   


MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HENRY JUMA MKAZI WA MIGOMBANI ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KULAZWA KITANDANI NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA VENANCE.
TUKIO HILO LA KUSIKITISHA LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KATA YA MIGOMBANI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA AMBAPO BAADA YA UHALIFU HUO, MTUHUMIWA ALIFUNGA MLANGO KWA NJE NA KUFULI NA KUTOKOMEA MAHALI KUSIKOJULIKANA. WAPELELEZI PAMOJA NA RAIA WALIPOVUNJA MLANGO NA KUINGIA NDANI WALIKUTA MAITI YA MTOTO HUYO IKIWA KITANDANI. KATIKA CHUMBA HICHO WALIKUTA UJUMBE WA MANENO MENGI YALIYOANDIKWA NA MTUHUMIWA, BAADHI YA MANENO HAYO NI “UNYAMA UNYAMANI, TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI”. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
REY C BADO ALIA NA MADAWA YA KULEVYA JINSI YALIVYO MUATHILI.
Q Chillah asema hafanyi filamu kukimbia majukumu ya muziki  Mwimbaji wa bongo flava, Q Chillah ambaye hivi sasa anaonekana kuwa karibu zaidi na kiwanda cha filamu amesema kuwa kuingia kwenye tasnia hiyo haimaanishi kuwa amekimbia majukumu ya muziki.
Q Chillah ameiambia Bongo5 kuwa bado ana uwezo mzuri wa kuimba na ataendelea kufanya muziki na kwamba watu wanapenda afanye filamu japokuwa yeye sio mtu wa filamu.
“Japokuwa mimi sio mtu wa filamu lakini watu wengi wanapenda nifanye filamu. Kwa hiyo nashangaa baadhi ya watu wanadhani nimeenda kwenye filamu kwa ajili ya kuuza sura na kukimbia majukumu yangu ya muziki. Jamani mimi ni msanii mkubwa sana na nina uwezo mkubwa sana wa kuimba na kufanya vitu vizuri sana katika muziki.” Amesema Q Chillah.
“Kwa hiyo nitaendelea kufanya muziki wangu mzuri na kama nitahitajika kufanya filamu nitafanya. Lakini maisha yangu ya nyuma ya pazia naweza sana kufanya filamu vizuri sana, na pia si biashara.”
Ameeleza kuwa alifuatwa na JB na muongozaji Adamu Kuambiana wakamtaka afanya filamu ya ‘Hukumu ya Ndoa Yangu’ na kwamba JB alimwambia awe kwenye kampuni yake.
Credit:Bongo 5.
TOA MAONI alphamsigwa.blogspot.com

Hii ndio historia aliyoiandika Pep Guardiola baada ya Bayern Munich kutwaa ubingwaBAYERN-0111_600_396_100Kocha Pep Guardiola jana usiku aliandika historia akiwa na klabu ya Bayern Munich baada ya kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Bundesliga      10154423_10152099255323598_1013413957_n-1Historia aliyoandika Guardiola ni kuiongoza FC Bayern München kutwaa ubingwa wa 23 wa Bundesliga baada ya michezo 27 tu huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi – huu ndio ubingwa wa haraka zaidi katika historia ya Bundesliga.

Ubingwa huu ni wa tatu kwa Pep Guardiola katika msimu wake wa kwanza, alishinda UEFA Super Cup mwaka jana mwezi August, kisha wakashinda ubingwa wa klabu bingwa ya dunia December mwaka jana.
ad_116403401      Manchester United jana iliendeleza uteja wake kwa wapinzani wao Manchester City baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford, jana usiku.
Matokeo ya mchezo huo yalitengeneza rekodi nyingine mbovu za Manchester United chini ya kocha David Moyes na zipo kama ifuatavyo
*Kipigo cha jana usiku kinaamanisha United sasa imepoteza mechi ugenini na nyumbani dhidi ya Liverpool na Manchester City ndani ya msimu mmoja – haijawahi kutokea hii huko nyuma.
*Man United mpaka sasa imefungwa mechi 10 katika premier league – idadi kubwa zaidi katika historia yao – pia kati ya mechi hizo 10 sita wamefungwa Old Trafford – haijawahi kutokea katika miaka 12 iliyopita United kufungwa mechi sita za ligi kuu kwenye uwanja wake wa nyumbani.
*Mpaka sasa United imecheza 13 dhidi ya timu 9 za juu katika msimamo wa ligi – na kati ya hizo imeshinda mechi 1 tu dhidi ya Arsenal. STORY BY PRINCE ALPHA

Monday, March 17, 2014

BASI LAYANGA LATAKA KUMWAGA WATU PICHA NA PRINCE ALPHABus la timu ya Young Africans lililokuwa limebeba wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi limepata ajali eneo na Mikese Mizani baada ya Mabus yaliyokua...yakitanua kuelekea mikoa ya bara kuziba njia na kusababisha kutumbukia kwenye mtaro.
Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa na kwa sasa timu inaondoka na usafiri wa bus jingine kuelekea jijini Dar es salaam BY PRINCE ALPHA.

Baada ya Wema kudaiwa kumfanyia Diamond fujo studio, leo kaweka hii picha.Screen Shot 2014-03-15 at 11.55.14 AM            Kupitia Kipindi cha  HOT SHOW HIGHLANDS FM [92.7]March 14 2014 zilitoka stori kwamba Wema Sepetu amekwenda na kumfanyia fujo Diamond Platnumz studio.

Hiyo ilitokana na kuona video ya Diamond akiwa na Victoria Kimani studio, msichana ambae amewahi kutajwa kuwa mapenzini nae. STORY BY PRINCE ALPHA.


Hii hapa video mpya ya Izzo B.izzo1Izzo B ni miongoni mwa wasanii wanaowakilisha 92.7 HIGHLANDS Fm Mbeya hii ni video ya wimbo wake mpya uitwao Tummoghele ambapo upande wa audio yake ilitoka wiki chache zilizopita, STORY BY PRINCE ALPHA FROM 92.7




Chris Brown afukuzwa Rehab na kutupwa lupangoWakati jitihada za kumtibu Chris Brown ili aweze kudhibiti hasira zake zikiendelea, imeripotiwa kuwa mwimbaji huyo amefukuzwa Rehab na kuishia kwenye mikono ya polisi waliompeleka moja kwa moja polisi na kumtupa lupango.
Kwa mujibu wa ripoti za kitengo cha polisi cha Los Angeles, Chris Brown alikamatwa Ijumaa (March 14) baada ya kufukuzwa Rehab japo sababu za kufukuzwa Rehab hazikuwekwa wazi.
Kitengo hicho cha polisi kimeeleza kuwa Chris alikamatwa majira ya saa nane mchana na kwamba alitoa ushirikiano kwa polisi hao hadi alipofikishwa katika kituo cha polisi ambako aliwekwa mahabusu.
Kitengo hicho kimeeleza kuwa amekamatwa kwa warrant iliyotolewa kutokana na makosa ya kutumia silaha na kutishia katika tukio lililotokea February 7, 2009. Na pia kwenda kinyume na masharti ya probation iliyohusu kesi hiyo.
Huenda tarehe iliyotajwa na polisi imechanganywa kwa kuwa Chris alimpiga Rihanna February 8, 2009.
Hii sio mara ya kwanza kwa Chris kufukuzwa Rehab kwa kuwa aliwahi kufukuzwa baada ya kurusha jiwe lilipasua kioo cha dirisha la gari la mama yake.

Inasemekana kuwa wakati akiwa Rehab alianzisha uhusiano na mfanyakazi wa Rehab na huenda ndio chanzo cha kumuacha Karrueche Tran, japo hiyo sio sababu iliyompelekea kufukuzwa.  story by PRINCE ALPHA HIGHLANDS FM 92.7 NDO HABARI YA TOWN.