
Kwa mujibu wa ripoti za kitengo cha
polisi cha Los Angeles, Chris Brown alikamatwa Ijumaa (March 14) baada
ya kufukuzwa Rehab japo sababu za kufukuzwa Rehab hazikuwekwa wazi.
Kitengo hicho cha polisi kimeeleza
kuwa Chris alikamatwa majira ya saa nane mchana na kwamba alitoa
ushirikiano kwa polisi hao hadi alipofikishwa katika kituo cha polisi
ambako aliwekwa mahabusu.
Kitengo hicho kimeeleza kuwa
amekamatwa kwa warrant iliyotolewa kutokana na makosa ya kutumia silaha
na kutishia katika tukio lililotokea February 7, 2009. Na pia kwenda
kinyume na masharti ya probation iliyohusu kesi hiyo.
Inasemekana kuwa wakati akiwa Rehab
alianzisha uhusiano na mfanyakazi wa Rehab na huenda ndio chanzo cha
kumuacha Karrueche Tran, japo hiyo sio sababu iliyompelekea kufukuzwa. story by PRINCE ALPHA HIGHLANDS FM 92.7 NDO HABARI YA TOWN.
Huenda tarehe iliyotajwa na polisi imechanganywa kwa kuwa Chris alimpiga Rihanna February 8, 2009.
Hii sio mara ya kwanza kwa Chris
kufukuzwa Rehab kwa kuwa aliwahi kufukuzwa baada ya kurusha jiwe
lilipasua kioo cha dirisha la gari la mama yake.
No comments:
Post a Comment