
Mshindi wa tuzo kadhaa za muziki za Tanzania (KTMA 2013), Kala Jeremiah ambaye mwaka huu jina lake halikutajwa katika vipengele vyote vya kuwania tuzo hizo ametoa mtazamo wake kuhusu kutotajwa kwake.
Rapper huyo wa Rock City Mwanza amesema kuwa moyo wake uko sawa na anaona kila kitu kiko sawa na kwamba hana hata swali.
“Yaani
mimi sijui nikoje, nimezaliwa tofauti sana nadhani na binadamu wengine.
Yaani ni mtu fulani wa ajabu sana, naonaga kila kitu kiko sawa. Moyo
wangu uko tofauti sana, sina tatizo lolote yaani sijui nikwambieje…yaani
niko very comfortable na naona ni sawa kabisa sina swali sina chochote
kwenye moyo wangu niko vizuri. Naona ni Mungu aliniumba vizuri sana hivi
nilivyo kwa sababu kila kitu nakichukulia fresh.” Kala Jeremiah
aliniambia Tovuti ya Times Fm.
Ameeleza
kuwa anaona watu walioingia walistahili kuingia na kwamba hata mwaka
jana hakuwa anatarajia kuingia kwenye vipengele hivyo na hata kushinda,
kwa hiyo hata mwaka huu pia alikuwa hatarajii chochote.
“Ndio
maana nilipotajwa mwaka jana nikashtuka na hata nilipopata tuzo pia
nikashtuka. Yaani kila kitu mi nadhani kinatakiwa kije chenyewe kwa
sababu ukikifikiria kitu…mi naona hata kukifikiria kitu na kupanga eti
itakuwa hivi au itakuwa hivi, no. Sidhani kama hiyo ni njia sahihi, njia
sahihi mimi naona ni kufanya kazi nzuri na kuacha watu wafurahi na kazi
zako.” Ameongeza rapper huyo wa Wale Wale.
Kala
ameeleza kuwa hata wakati anashiriki mashindano ya BSS hakuwa na
wasiwasi wa kuendelea ama kutoendelea na mashindano kwa kuwa kwake yeye
huona kila kinachotokea katika hali hiyo ni sawa.
Wimbo
wa Dear God uliotayarishwa na Dee Classic ulimpa tuzo tatu muhimu mwaka
jana ikiwa ni pamoja na tuzo kubwa ya wimbo bora wa mwaka. Alishinda
pia tuzo ya msanii bora wa hip hop akiwabwaga Fid Q, Joh Makini, Profesa
Jay na Stamina.
Kala
aliitoa tuzo ya wimbo bora wa hip hop na kumkabidhi mama yake Albert
Mangwea kwa heshima na kumuenzi rapper huyo aliyefariki May 28 mwaka
jana nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment