Hii ndio historia aliyoiandika Pep Guardiola baada ya Bayern Munich kutwaa ubingwa
Kocha Pep Guardiola jana usiku aliandika historia akiwa na klabu ya
Bayern Munich baada ya kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Bundesliga
Historia aliyoandika Guardiola ni kuiongoza FC Bayern München kutwaa
ubingwa wa 23 wa Bundesliga baada ya michezo 27 tu huku wakiwa
hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi – huu ndio ubingwa wa haraka
zaidi katika historia ya Bundesliga.
Ubingwa huu ni wa tatu kwa Pep Guardiola katika msimu wake wa kwanza,
alishinda UEFA Super Cup mwaka jana mwezi August, kisha wakashinda
ubingwa wa klabu bingwa ya dunia December mwaka jana.
No comments:
Post a Comment