
Q
Chillah ameiambia Bongo5 kuwa bado ana uwezo mzuri wa kuimba na
ataendelea kufanya muziki na kwamba watu wanapenda afanye filamu
japokuwa yeye sio mtu wa filamu.
“Japokuwa
mimi sio mtu wa filamu lakini watu wengi wanapenda nifanye filamu. Kwa
hiyo nashangaa baadhi ya watu wanadhani nimeenda kwenye filamu kwa ajili
ya kuuza sura na kukimbia majukumu yangu ya muziki. Jamani mimi ni
msanii mkubwa sana na nina uwezo mkubwa sana wa kuimba na kufanya vitu
vizuri sana katika muziki.” Amesema Q Chillah.
“Kwa
hiyo nitaendelea kufanya muziki wangu mzuri na kama nitahitajika
kufanya filamu nitafanya. Lakini maisha yangu ya nyuma ya pazia naweza
sana kufanya filamu vizuri sana, na pia si biashara.”
Ameeleza
kuwa alifuatwa na JB na muongozaji Adamu Kuambiana wakamtaka afanya
filamu ya ‘Hukumu ya Ndoa Yangu’ na kwamba JB alimwambia awe kwenye
kampuni yake.
Credit:Bongo 5.
No comments:
Post a Comment