Monday, August 25, 2014

Epl: Matokeo na wafungaji wa mechi ya Liverpool vs Man City haya hapa

IMG_6728.JPG
Wakati wakimtambulisha Mario Balotelli kuwa mchezaji wao mpya, klabu ya Liverpool leo ilikuwa wageni wa Manchester City katika dimba la Etihad kwenye mchezo wa ligi kuu ya England.
Wakiuanza mchezo huo kwa kasi Liverpool imejikuta ikifungwa magoli 3-1 na City.
Huku Balotelli akiwa jukwaani akiangalia timu yake ya zamani ikitoa kipigo hicho kwa Liverpool, walikuwa ni Stevan Jovetic aliyefunga magoli mawili na Sergio Kun Arguero waliopeleka kilio Anfield.
Goli la kujifunga la Zabaleta likawafuta machozi vijana wa Brendan Rogers.
Mpaka filimbi ya mwisho matokeo yalikuwa 3-1.

No comments:

Post a Comment