SAFARI YA MWISHO YA MZEE MALANGALILA, MWANAHABARI MKONGWE MKOANI IRINGA
Mwili wa Mzee Fulgence Malangalila, mwandishi wa habri mkoangwe mkoani Iringa ukiwa nyumbani kwake, Frelimo mjini Irimga
Mzee Malangalila enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa nyumbani, kwa mzee Malanalila...
MWANAHABARI mkongwe mkoani Iringa, Fulgance Malangalila (71) amefariki dunia, baada ya kulazwa kwa takribani wiki moja katika hospitali ya mkoa wa Iringa.
Jitihada za madaktari wa hospitali hiyo kunusuru maisha ya Malangalila aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukuri kwa muda mrefu zilishindikana.
Kabla mauti hayajamkuta, Malangalila alikuwa mwandishi wa kujitegemea akiandika uchambuzi na makala katika vyombo mbalimbali vya habari nchini yakiwemo magazeti ya Business Times na Majira
Ndani ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, Malangalila alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu akiongoza kamati ndogo ya maadili.
Malangalila anazikwa mchana huu katika makaburi ya Tosamaganga, nje kidogo ya mji wa Iringa.
No comments:
Post a Comment