Stori kuhusu helikopta ya Dr. Slaa na Mnyika kutaka kulipuliwa Shinyanga.
Naibu
Waziri wa Nishati ametajwa kwenye njama za kutaka kumuua Katibu mkuu wa
CHADEMA Dr. Slaa pamoja mbunge wa Ubungo John Mnyika kwa kuilipua
Helikopta wanayosafiria.Magazeti ya Tanzania August 9 2014 kama Tanzania Daima na Nipashe yameripoti kwamba Naibu Waziri huyo anadaiwa kupanga njama za kuilipua Helikopta ya Dr. Slaa na Mnyika wakiwa ziarani mkoani Shinyanga kukusanya maoni ya Wananchi juu ya muundo wa serikali mkoani Shinyanga.
Tuhuma hizo zilitolewa na diwani wa kata ya Ngokelo Sebastian
Peter kutoka Shinganga ambae anasema yeye na mwenzake Zakaria Mfukwa
waliahidiwa shilingi milioni 180 kila mmoja kwa ajili ya kuikamilisha
hiyo kazi na walipewa kazi hiyo ya kutoa taarifa zote kuhusu kutua kwa
Helikopta hiyo na kazi ya ulipuaji ingesimamiwa na Waziri mwenyewe
ambayo hata hivyo haikufanikiwa.Kupata kila stori inayonifikia mtu wangu niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB
No comments:
Post a Comment