Watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi wamemteka na kumvamia mwalimu mmoja na
kumpora kiasi cha zaidi ya Sh milioni 20 na kisha kumbaka mwalimu
mwingine wa kike katika kijiji cha Nassa Ginery wilayani Busega mkoani
Simiyu.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Simiyu, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi kijijini hapo.
Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Simiyu, Evance Mwijage ndiye
aliyethibitisha kuwapo kwa tukio hilo alipozungumza na mwandishi wa
habari hizi kwa njia ya simu.
Hata
hivyo, hakuwa tayari kuelezea zaidi taarifa juu ya tukio hilo, akisema
alikuwa anasubiri jalada la Polisi kutoka wilayani Busega ambalo lina
taarifa za kina, ikiwa ni pamoja na watu wanaohusishwa na tukio zima.
Lakini
kwa upande wa mwalimu aliyetekwa na kuporwa fedha, Samwel Mbochi
alisema siku ya tukio, watu anaoamini kuwa ni majambazi waliruka ukuta
wa nyumba yake na kumvamia na kumshikilia wakimtaka atoe pesa.
Anasema
alitii amri yao na kutoa kiasi hicho cha fedha alichokuwa amekiandaa
kwa ajili ya kununua bidhaa kesho yake, kwani pamoja na kuwa mwalimu,
pia amekuwa akijishughulisha na biashara ya duka kijijini hapo.
Anaongeza
kuwa, baada ya kuchukua fedha, walivamia chumba kingine cha mwalimu wa
kike ambaye ni mpangaji wake na kumbaka kwa zamu, kisha kutokomea
kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment