Tuesday, November 12, 2013

Dk. Sengondo Mvungi amefariki dunia katika Hospitali ya Milpark Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Dk. Mvungi alipelekwa wiki iliyopita Nov. 7 kwa ajili ya kupewa matibabu zaidi akitokea Hospitali ya Muhimbili kitengo cha Moi ambako muda wote alikuwa hajitambui baada ya kushambuliwa na majambazi na kuumizwa vibaya sehemu ya kichwani akiwa nyumbani kwake Kibamba.

Wakati Dk. Mvungi anafariki, jana Jeshi la Polisi, kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, lilitangaza kuwakamata watuhumiwa 9 wakiwa na mapanga yaliyotumika katika uvamizi huo.


MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI - AMEEN!. MATUKIO YOTE YAKIRATIBIWA NA ALPHA MSIGWA THE PRINCE 
  R . I. P

No comments:

Post a Comment