WANAIGERIA WAMWEKA KITI MOTO DIAMOND KWA KUVAA VIBAYA KWENYE ARUSI YA PETER WA P-SQUARE MA2KIO NA PRINCE ALPHA.
So Diamond Platnumz jana alikuwa
miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria harusi ya kimila ya Peter
Okoye wa kundi la P-Square na mchumba wake, Lola Omotayo iliyofanyika
jijini Lagos, Nigeria.
Kwenye harusi hiyo, Diamond alipata
nafasi ya si tu kushuhudia Peter na Lola wakisema ‘Yes I do’ bali pia
aliweza kuchill na cream ya mastaa wa Afrika wakiwemo Iyanya na mchezaji
wa timu ya Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Togo, Emmanuel
Adebayor.
Alipata pia fursa ya kuwaonesha Adebayor na Iyanya style yake ya kucheza ya Ngololo
Hata hivyo, kitu kimoja hakikwenda sawa.
Ni nguo aliyokuwa ameivaa, ambayo iligeuka gumzo kwa mashabiki wengi wa
muziki nchini Nigeria waliosema kachemka. BY ALPHA MSIGWA 0764849514
No comments:
Post a Comment