
1.
‘Kimsingi nimeonyesha msimamo kwamba nampinga kwa sababu hatendei haki
chama na ndio msimamo wa kamati kuu, tunachoamini ni kwamba tunatakiwa
kupigana wote… kwenye matukio yote muhimu yenye maana ambayo ni ya
kukijenga chama hatujashirikiana nae, hatujalia pamoja hatujafurahi
pamoja, wenzake tulifurahi pamoja Tarime hakuwepo, tumelia pamoja Arusha
wenzake wote mara mbili, Iringa, Morogoro hajakuwepo’
2.
‘Bungeni tumedharauliwa tumetukanwa kwenye matukio yote haya ya msingi
hajakuwepo lakini kibaya zaidi amekuja na Waraka huu ambao amefanya na
mwenzake Kitila, Waraka wa kukigawa chama kwa hiyo mambo kama haya ndio
nimeamua kuonyesha msimamo wangu hadharani na naamini Wabunge wengine
ambao tuko nao wataendelea kujitokeza siku zinazokuja kwamba hatuko nae
kwenye swala hili hata yeye mwenyewe nimeshaongea nae uso kwa uso,
sijali nani ni nani… i don’t care’
3.
‘Mimi ni bora nichukiwe katika uhalisia, sitaki kupendwa kinafiki kama
mtu ananichukia ni sawa lakini msimamo wangu ndio huo na kwamba Zitto
Kabwe hastahili kuwa Naibu Katibu mkuu wa chama chetu’
STORY BY PRINCE ALPHA

No comments:
Post a Comment