Thursday, July 17, 2014












HABARI;
Mtoto mwenye umri wa miaka minane (Jina limehifadhiwa) anadaiwa kufanyiwa kitendo cha kulawitiwa na mtu mmoja ambaye amemtaja kuwa ni mwendesha Bodaboda ya baiskeli.Katika maelezo yake mtoto huyo anadai akiwa anatoka shule na mwenzake njiani walisimama wakawa wanaokota matunda(Ntalali)ghafla mtuhumiwa alitokea na kumtaka mtoto huyo ampeleke nyumbani kwao kwakuwa alikuwa wakifahamiana kabla ya hapo.
Mtoto alisema alikubali kuondoka na bwana huyo na kupakizwa kwenye baiskeli hadi eneo la maficho karibu na mlima na ndipo alianza kufanyiwa kitendo hicho.Baada ya kurejea nyumbani mtoto huyo alimweleza mama yake mzazi na kuanza harakati za kufika kituo cha Kikubwa cha Polisi.Hatua za kumkamata mtuhumiwa zilifanyika ingawa aliachiwa kwa dhamana jambo ambalo mama mzazi wa mtoto huyo amelilalamikia huku akidai kuwa huenda kuna hujuma dhidi ya kitendo kibaya alichofanyiwa mtoto wake.

No comments:

Post a Comment