
Mshambuliaji wa Uholanzi na Bayern Munich Arjen Robben, 30, amekataa 'ofa' ya kujiunga na meneja wake Louis van Gaal, Old Trafford (Daily Telegraph).
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana matumaini ya kukamilisha usajili wa kipa wa Colombia David Ospina, 25, kutoka klabu ya Nice wiki hii (Daily Mirror).
Chelsea wameanza mazungumzo kuhusu kumrejesha Didier Drogba, 'Darajani' kuwa mshambuliaji wa akiba na kocha (Daily Mail), mshambuliaji wa Liverpool Iago Aspas, 26, anajiandaa kujiunga na Sevilla kwa mkopo msimu wote ujao (Liverpool Echo), mipango ya uhamisho ya Tottenham imekwama kwa sababu kiungo Gylfi Sigurdsson, 24 na beki Michael Dawson, 30, hawataki kuondoka (Daily Mirror), wakala wa beki wa Spurs Jan Vertonghen, 27, amekiri kuwa mchezaji huyo huenda akaondoka White Hart Lane (Evening Standard), Liverpool wameanza tena kumfuatilia beki wa kushoto wa Sevilla Alberto Moreno (Daily Express)(P.T)
No comments:
Post a Comment