Mwizi baada ya kuingia ndani akakosa cha kuiba, lakini pembeni aliona chungu kilikuwa na unga wa muhogo.
Jamaa akaona sio haba bora achukue chochote; akavua shati lake akalitandika chini akasogea kwenye chungu cha unga ili aumiminie kwenye shati alilolitandika chini ili aubebe kirahisi bila kuondoka na chungu, kumbe mwenye nyumba anamuona.
Jamaa alivyogeuza mgongo tu kuchukua chungu, kwa kasi ya umeme baba
mwenye nyumba aliliiba lile shati na kurudi chumbani fasta, mwizi
aliporudi alipolitandaza shati hakulikuta, akaguna kwa sauti Mhhh!
Mke wa mwenye nyumba akumuuliza mumewe kama naskia kuna mwizi, jamaa akamwambia hakuna mwizi tulale tu! Mwizi akapiga kelele hapana mwizi yupo mbona shati langu silioni!!
Mke wa mwenye nyumba akumuuliza mumewe kama naskia kuna mwizi, jamaa akamwambia hakuna mwizi tulale tu! Mwizi akapiga kelele hapana mwizi yupo mbona shati langu silioni!!
No comments:
Post a Comment