
Abiria
37 na wafanyakazi 4 wa ndege ya Precision Air wamenusurika kifo baada
ya ndege waliyokuwa wamepanda kupasuka matairi wakati ikitua katika
uwanja wa ndege wa Arusha leo majira ya mchana.
Waziri
mkuu mstaafu ambaye ni mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alikuwa
miongoni mwa abiria wa ndege hiyo waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es
Salaam kwenda Arusha.
Shirika
la ndege la Precision Air limetoa tamko rasmi kwa umma, ambapo
limeeleza kuwa watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wako salama.

No comments:
Post a Comment