Tuesday, December 17, 2013


Yanga kuhusu Okwi tenaokwi


Kumekuwa na maneno mengi sana mtaani tangu mshambuliaji Emanuel Okwi ajiunge na club ya Dar Young African.
Haya ndo maneno ya Yanga kuhusu Okwi  ‘Simba walikua wanasema Yanga tuna wachezaji 29 nadhani walikua hawatambui,usajili mkubwa tuliofanya ulikua na wachezaji 27 akiwemo Omeja Sene ambae tulimpeleka kwa mkopo kwenye timu ya Prison,kwa hiyo tulikua na nafasi 3 za kujaza ikiwemo nafasi moja ya mchezaji wa kimataifa kwa hiyo tulitumia nafasi hiyo kumuongeza Juma Kaseja na Hassan Dilunga wakiwa kama wazawa lakini pia tumekamilisha utaratibu wa kumsajili mshambuliaji Emanuel Okwi kutoka nchini Uganda katika club ya Villa na tumefikia hatua hii ya kutangaza baada ya kukamilisha na kupata hati zote ikiwa ni pamoja na hati za uhamisho wa kimataifa ambayo inatolewa na shirikisho la soka husika na kutufikia sisi kwa hiyo napenda kuwatambulisha rasmi kama Emanuel Okwi ni mchezaji halali wa club ya Yanga na usajiri wake tumeshauwasilisha na tunatazamia ndani ya siku mbili hizi atakuja kujiunga na wenzake kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili na mashindano ya ligi ya club bingwa ya Africa.

No comments:

Post a Comment