Unaamini huyu mshkaji kafanana na Marehemu Ngwea kwa asilimia 100?
Tamasha la Xxl Afta xkul Bash ndio sehemu ambayo nilimuona huyu
jamaa baada ya kujitokeza kwenye mashindano ya kumtafuta Mtu anaefanana
na Star.Nikaona si mbaya tukafahamu hata kwa uchache historia yake na anamjua vipi Marehemu Ngwea.
Mi naitwa Mohamed au Junior weezy, junior weezy kwa sababu imekua
Talk of Town gumzo Town kila mtu Ngwea Ngwea,mi Ngwea namfaham kama
artist so nimeonana nae mara ya mwisho nikiwa mdogo lakini Jay Moe
alimwambia Ngwea unafanana sana na jamaa pale ndo ilikua mara yangu ya
kwanza naya mwisho kuonana na Ngwea’.
Yeah ilikua mwaka 2003 baada ya Jay Moe kumwambia unafanana sana na
dogo alisema ndio kweli nafanana nae lakini mtu aliekuja kunifahamisha
zaidi ni Dully,Dully alisema unafanana sana na Ngwea na mpaka leo huwa
ananiita Ngwea.watu walinishawishi kulingana na hii sura nliyonayo watu
wamenishawishi taratibu naanza kuingia kwenye game bado sijafanya track
nipo njiani,nakutana na vituko vingi wengine wananikimbia wanasema
nimefufuka na vitu vingine vya ajabu nakutana navyo mtaani muda mwingine
nasisimka nahisi kama Mangwea yuko ndani ya mwili wangu,naweza kuimba
baadhi ya ngoma za Ngwea kama tupo juu..na baadhi ya ngoma zingne.

No comments:
Post a Comment