
Watengezaji
wa filamu wamekuwa wakivutiwa na maisha na historia ya Nelson Mandela
katika kupambana na ubaguzi wa rangi kabla hajatoka jela mwaka 1990.
Na baada ya kuwa Rais wa Afrika Kusini historia yake ikawa ya kuvutia zaidi.
Alhamis, kiongozi huyo anayependwa duniani alifariki dunia na kuiacha dunia ikivutiwa na vitendo vyake vya kusamehe na umoja.
Kumuigiza Mandela si kazi rahisi kwa waigizaji. Hata hivyo hizi ni filamu 6 zilizoigiza maisha yake.
Idris Elba kwenye Mandela: Long Walk to Freedom.Idris Elba amepata sifa za mapema kwa kuigiza filamu ya Mandela: Long Walk to Freedom. Ili kufanya utafiti zaidi kwenye uhusika huo, Elba aliliambia shirika la Associated Press kuwa alikutana na mke wa pili wa Mandela, Winnie, aliyemuambia kuwa alihitaji kuona mwanaume mkakamavu kwenye screen, STORY BY PRINCE ALPHA
No comments:
Post a Comment