
Kwenye
hizi siku mbili tatu headlines za Magazeti, blogs, website na vyanzo
vingine vya habari zimemilikiwa pia na habari kuhusu Diamond Platnumz na Baby Madaha kuhusu kurushiana maneno baada ya kauli ya kwanza ya Baby.
Madaha
amezungumza ya moyoni on millardayo.com baada ya kusambaa kwa taarifa
hizi na kufafanua kwamba ‘kiukweli ni kwamba hakuna ugomvi wowote labda
ni yeye anaukuza ama ni nini, mimi sina ugomvi nae wala sitaki…
nilichoongea ni ukweli kwamba alikua hajui muziki, uwezo wake huwezi
kuulinganisha na Barnaba au Ali Kiba, nilitoa maoni yangu so haina haja
ya kusema ni chuki’
‘Ukweli
siku zote watu wanauogopa so sijali atajibu nini kwa sababu niko tayari
kumjibu na nitasimamia kwenye point yangu na yeye kama ataongea aongee,
muziki hauna Mungu mtu wa kusema kwamba asiambiwe kitu chochote hata
kama anakosea, hata kama anaiba mashairi ya watu wengine asiambiwe? hata
kama wimbo wake sio mzuri asiambiwe? tunahitaji changamoto kwenye
muziki’ – Madaha
Kwa
kumalizia, Madaha anasema ‘aumize kichwa kama wenzake na aweze kufanya
muziki vizuri ambao hautategemea kiki kupitia skendo za mapenzi,
asijiweke sana kweye skendo ili watu waelewe uwezo wake binafsi Diamond
kama Diamond, so hiyo haikua beef… ni ukweli na ukweli uauma na
kuogopwa, ndio maana akareact’
STORY BY ALPHA MSIGWA aka THE PRINCE aka IGP SAID PLAY BOY MWEMA.

No comments:
Post a Comment