
Nchini
England mabingwa watetezi wa Ligi ya nchi Hiyo Manchester United
wameendelea na mwanzo mbaya wa ligi hiyo baada ya hii leo kukubali
kipigo cha bao moja bila toka kwa Newcastle United .
Bao
pekee lililoacha simanzi kwa mashabiki wa United lilifungwa na kiungo
Mfaransa Yohan Cabaye. Matokeo haya yanaiacha United kwenye nafasi ya
tisa wakiwa wameachwa na vinara wa ligi hiyo kwa pointi 12.
Hii
ni mara ya kwanza kwa United kupoteza mechi mbili mfululizo kwenye
uwanja wake wa nyumbani tangu mwaka 2002 huku ikiwa ni mara ya kwanza
kwa Newcastle United kushinda mchezo kwenye uwanja wa Old Trafford kwa
miaka 41.
No comments:
Post a Comment