Kijana mmoja ashambuliwa hadi kufariki dunia baada ya kusemekana kwamba ni mchawi aliyedondoka na ungo.Wananchi wakiwa hasira kali wamempiga hadi kumuua mwanaume
aliyedhaniwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo
ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.
Jamaa huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka
20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo ya Mbezi Luis baada ya
kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.
Mashuhuda wanasema kabla ya kufariki alisema “Mimi nilikuwa na
wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa
tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”
“Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu
kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii
inayopelekea mauti yangu”
Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo
wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa
hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka
kwao.
No comments:
Post a Comment