Leo
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe amehutubia wananchi wake wa
Kigoma kwa mara ya kwanza mkoani hapa tangu avuliwe nyadhifa zake zote
ndani ya chama chake cha Chadema.Zitto alifika kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma saa tatu asubuhi na
kufuatiwa na maandamano yaliyoanzia ofisi ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema kwenda kusaini kisha yakaendelea mpaka kijijini kwao
Mwandiga mchana wa leo na kufuatiwa na mkutano wa hadhara uliohudhuriwa
na mamia ya wananchi wa eneo hilo wakiwa wamebeba Mabango mbalimbali.Miongoni mwa mabango hayo yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao
kuna yaliyosomeka Zitto Kama Nyerere, Zitto kama Mandela Kasoro Jela,
Zitto rais wetu 2015,waha siyo nguruwe,karibu mwamba wa siasa,Zitto kama
Nyerere,Mandela wa Tanzania karibu Kigoma na mengine mengi.Akihutubia mamia ya wananchi waliokusanyika kwenye uwanja Mwandiga
Zitto alisema mwaka 2006 wananchi wa Kigoma mlifanya tena maandamano
na mapokezi kama haya mlipokuwa mnanipokea baada ya kusimamishwa ubunge
na wana CCM nilipokuwa natetea maslahi ya wananchi, safari hii hali hii
imetokea kutokana na changamoto nilizonazo kwenye chama changu.
No comments:
Post a Comment